Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MTANZANIA Kema Salum (39) amehukumiwa kifungo cha miaka 23 gerezani baada ya kukutwa na hatia ya kumuua mkewe Leyla Mtumwa (35) wakiwa nyumbani kwao katika kitongoji cha  Haringey,  Kaskazini ya  Uingereza mnamo mwezi Machi mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa katika tovuti ya BBC, Mahakama  imeeleza kuwa chanzo cha tukio hilo ni Salum kuwa na wivu wa kimapenzi kwa mkewe mara baada ya mkewe huyo kutoka na rafiki zake usiku, mahakama ilielezwa.
Kema amekuwa akiishi Uingereza kwa visa ya miezi sita tangu waoane na Leyla  nyumbani Tanzania kabla ya kumtoa roho.
Imeelezwa kuwa mapema Machi 30 mwaka huu, Salum alianza kwa mashambulizi makali kwa kumkaba kabali mkewe huyo mida ya saa moja nyumbani kwao Kirkstall Avenue. 
Mahakama ilielezwa kuwa Kema alisitisha kwa muda  shambulizi hilo na kwenda jikoni na kurudi na kisu ambacho alikitumia kumchoma Leyla kichwani, shingoni, mwilini na mikonononi mara 49  huku mtoto wao kiume wa umri wa miaka 12 akishuhudia na kupiga kelele akimzuia baba yake, bila mafanikio, mahakama iliambiwa.
Aidha imeelezwa kuwa awali alikana kufanya mauaji hayo kwa kusema kuwa alikuwa anajilinda, lakini mnamo mwezi  mwezi Septemba akakiri kufanya mauaji hayo. Mahakama iliambiwa kwamba Salum alikuwa na tabia ya ukali uliopindukia kwa mkewe siku za nyuma.
Jaji Richard Mark QC alieleza kwamba mshtakiwa alikuwa mtu jeuri, mwingi wa ubabe kumbana mkewe. 
"Shambulio hilo lilikuwa si la kwanza na lenye kutumia mabavu sana ambayo, japo lilikuwa la muda mfupi, bila shaka lilimsababishia Leyla maumivu makali kabla ya kukata roho", alisema Jaji Richard.
Kachero mpelelezi Inspekta Dave Whellams aliyeongoza uchunguzi wa tukio hilo, amesema sababu hasa ya Salum kufanya kitendo hicho cha kikatili haijulikani bado.
"Inasikitisha kwamba huenda tusiweze kujua ni nini hasa kilichotokea cha  kusababisha shambulio hilo. Hata hivyo, nategemea hukumu ya leo italeta hitimisho la faraja  kwa familia ya Leyla", Inspekta Whellams alisema.
 Marehemu Leyla Mtumwa
Mshtakiwa Kema Salum.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...