Watu
saba waliokuwa wakisafiri katika gari STL 6250 mali ya CAG wamekufa
papo hapo na wengine watatu kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa
wakisafiria kugongana uso kwa uso na gari SU 41173 mali ya PSSSF, katika
eneo la Chalinze Mkoani Dodoma leo.
Taarifa
za awali zinaeleza kuwa waliofariki katika ajali hiyo mkoani Dodoma leo
katika gari la Ofisi ya CAG ni dereva wa ofisi hiyo na wengine 6 ni
ndugu wa Naibu CAG waliokuwa wakitoka katika msiba huko Chato mkoani
Geita.
Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma Giles Muroto, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba watu saba wamefariki katika ajali iliyohusisha magari mawili ya serikali ikiwemo, STL 6250 Toyota Land Cruiser kutoka ofisi ya CAG, baada ya kugongana uso kwa uso na gari yenye nambari SU 41173.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...