Na Mathias Canal-WK,
Mtwara
Wakulima wa zao la korosho wa Wilaya ya Tandahimba na Masasi wamekubali
kuuza korosho zao mbele ya Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) kutokana
na kuridhia na kukubaliana na maamuzi ya serikali.
Hayo yamejili katika mnada wa nne wa msimu wa uuzaji korosho
2018/2019 uliojumuisha kampuni za ununuzi 11 katika maghala tofauti uliofanyika
katika kijiji na kata ya Mdimba Mkoani Mtwara.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika
kijiji na kata ya Mdimba, Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba alisema
kuwa bei ya zao la korosho imeonyesha mwelekeo wa kushuka katika mwaka
2018/2019 tofauti na hali ilivyokuwa katika msimu wa mwaka 2017/2018 ambapo bei
ya zao hilo ilifikia shilindi 4,128
Katika mkutano huo wakulima wa korosho walikubali mbele ya
waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Tizeba kuanza kuuza korosho zao kwa bei ya juu ya
shilingi 3,016 huku bei ya chini ikiwa ni shilingi 3000.
“Wafanyabiashara wasipangiwe muda wa kuchukua korosho ghalani
kwa ajili ya usafirishaji na wasipangiwe kutumia bandari gani, wawe huru
kulingana na maagizo yaliyotolewa na Rais Magufuli’’
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mnada wanne wa msimu wa uuzaji korosho 2018/2019 wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji na kata ya Mdimba Mkoani Mtwara jana tarehe 2 Novemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mnada wanne wa msimu wa uuzaji korosho 2018/2019 wakimsikiliza kwa makini waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza katika kijiji na kata ya Mdimba Mkoani Mtwara jana tarehe 2 Novemba 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mnada wanne wa msimu wa uuzaji korosho 2018/2019 wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji na kata ya Mdimba Mkoani Mtwara jana tarehe 2 Novemba 2018.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mnada wanne wa msimu wa uuzaji korosho 2018/2019 wakimsikiliza kwa makini waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza katika kijiji na kata ya Mdimba Mkoani Mtwara jana tarehe 2 Novemba 2018.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...