Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna DCP Liberatus Sabas, katikati akiwa amenyanyua silaha aina ya AK 47 zilizopatikana katika Operesheni maalum ya kupambana na uhalifu iliyofanyika kuanzia Octoba mwaka huu mpaka Novemba mwaka huu katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma.
Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna DCP Liberatus Sabas, katikati akiwa amenyanyua Bomu moja (1) la kurushwa kwa mkono (Hand Grenade – Defensive) lililoko mkono wa kulia na milipuko mingine iitwayo Explosive – Gel V6 iliyokamatwa katika Operesheni maalum ya kupambana na uhalifu iliyofanyika kuanzia Octoba mwaka huu mpaka Novemba mwaka huu katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma.
Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna DCP Liberatus Sabas, katikati akionyesha mbolea aina Ammonium Nitrate na Potassium Nitrate zinazotumika kutengenezea milipuko mbalimbali, mbolea hizo zilipatikana katika Operesheni maalum ya kupambana na uhalifu iliyofanyika kuanzia Octoba mwaka huu mpaka Novemba mwaka huu katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma. (Picha na Jeshi la Polisi).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ninajitokeza kulisifu jeshi la polisi kwa kazi hiyo. Jeshi la polisi linastahili sifa linapofanya mambo ya aina hiyo ambayo yanaendana na wajibu na maadili yeke. Yanaleta heshima kwa jeshi. Lakini nawajibika kusema kwamba jeshi linajiharibia heshima pale linapotumika kisiasa kwa katika miaka hii ya vyama vingi. Tatizo hili lilianza zamani kiasi. Mwaka 2001, wakati wa machafuko Visiwani, tatizo lilijitokeza, na mashirika ya kutetea haki za binadamu yaliyoko ndani ya nchi na nje (kama vile "Human Rights Watch",) yaliandika taarifa juu ya tatizo hilo. Tatizo limeendelea, na tumefikia hatua ya kumsikia afande akihamasisha mkutano wa hadhara kwa kusema "Kidumu Chama cha Mapinduzi." Mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa, na sioni kama ni sahihi kwa polisi kutamka namna hiyo kuhusu chama chochote. Ninarudia kauli yangu kwamba ninaliheshimu na kulipongeza jeshi la polisi kwa mambo kama haya yaliyoripotiwa hapa. Na kwa kuwa ninaliheshimu, na ninataka libaki na sifa safi, ni lazima nitoe neno pale ninapoona linajiharibia taswira yake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...