Na Mwandishi Wetu,MAELEZO,DAR ES SALAAM.
SERIKALI imesema itaendelea kuweka
mazingira wezeshi na kuimarisha misingi ya haki na wajibu ya waandishi
wa vyombo vya habari nchini ili kuwawezesha kutekeleza vyema majukumu
yao yaliyoanishwa katika Mikataba na Sheria mbalimbali za kitaifa na
Kimataifa.
Hayo yamesema leo Jumamosi
(Desemba 22, 2018) Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Habari
(MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi wakati
akifungua warsha ya siku moja kwa waandishi na wahariri wa vyombo vya
habari iliyoandaliwa na Jumuiya ya Waislamu ya Shia Ithsheriya.
Dkt. Abbasi alisema kwa kuzingatia
Mikataba na Sheria mbalimbali za Kimataifa ikiwemo Kifungu cha 19 cha
Mkataba wa Kimataifa Haki za Kisiasa na Kiraia wa mwaka 1966, Serikali
imechukua hatua mbalimbali za kiutendaji ili kuhakikisha maboresho na
tasnia ya habari na utangazaji inapiga kubwa za maendeleo.
Kwa mujibu wa Dkt. Abbasi alisema
moja ya mafanikio ya Serikali ni pamoja na kutungwa kwa Sheria
mbalimbali ikiwemo Sheria ya Huduma za Habari na Sheria Haki ya Kupata
Taarifa ambazo kwa kiasi zimeweka mazingira wezeshi ikiwemo kuwepo kwa
vipengele vya kisheria zinazopaswa kutekelezwa na Taasisi za umma na
Binafsi katika utoaji na upatikanaji wa taarifa kwa umma.
Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnsheria Tanzania (T.I.C) Shekhe Hemmed Jalala akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari –MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi mara baada ya kuwasili katika semina ya Jukumu la Mwanahabari iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambako Dkt. Abbasi alikuwa Mgeni Rasmi.

Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnsheria Tanzania (T.I.C) Shekhe Hemmed Jalala( wa tatu kulia) akitoa moja ya maada zilizokuwa zikijadiliwa kwenye Semina ya Jukumu la Mwanahabari iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam, kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kutoka Ofisi ya Shekhe Mkuu wa Tanzania, Haris Othmani na Kushoto ni `Mkurugenzi Mkuu TAMWA Eda Sanga, Mwanyekiti wa Blogu (Bloggers ) Joachim Mushi, Mwenyekiti Msaidizi T.I.C Ramadhani Mlekwa na Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari –MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi wakifuatilia semina hiyo.

Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnsheria Tanzania (T.I.C) Shekhe Hemmed Jalala akisisitiza jambo kwa washiriki wa semina ya Jukumu la Mwanahabari wakati wa utoaji maada katika semina hiyo iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam

Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnsheria Tanzania (T.I.C) Shekhe Hemmed Jalala akisisitiza jambo kwa washiriki wa semina Jukumu la wanahabari wakati wa utoaji maada katika semina hiyo iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam, kulia ni Mwenyekiti Msaidizi T.I.C Ramadhani Mlekwa na Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari –MAELEZO Dkt. Hassan Abbasi wakifuatilia semina hiyo.

Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari –MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akitoa hotuba fupi kuhusu maada ya uhuru wa habari kwa mwandishi katika Semina ya Jukumu la Mwanahabari iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnsheria Tanzania (T.I.C) Shekhe Hemmed Jalala akifuatilia hotuba hiyo.

Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari –MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akisisitiza jambo kuhusu maada ya uhuru wa habari kwa mwandishi katika Semina ya Jukumu la Mwanahabari iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnsheria Tanzania (T.I.C) Shekhe Hemmed Jalala akifuatilia hotuba hiyo na kushoto ni Mwenyekiti Msaidizi T.I.C Ramadhani Mlekwa wakifuatilia maada hiyo.

Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari –MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa dini pamoja na watoa maada katika Semina ya Jukumu la Mwanahabari iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.(Picha na Idara ya Habari-MAELEZO)



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...