Na Teresia Mhagama, Njombe
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewataka wakandarasi wanaosambaza umeme vijijini kutochelewesha utekelezaji wa miradi hiyo kwa kisingizo cha mabadiliko ya hali ya hewa kama vile uwepo wa mvua. Aliyasema hayo wilayani Makete mkoani Njombe wakati alipokuwa akikagua kazi ya usambazaji umeme vijijini inayotekelezwa kupitia mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) mzunguko wa kwanza.
“ Kabla ya Serikali kuwakabidhi kazi hii ya usambazaji umeme vijijini, mlishafanya upembuzi wa maeneo mnayoenda kufanyia kazi na mnayafahamu vizuri, hivyo basi, iwe Jua au mvua, tunataka kuona kazi hii inaendelea kutekelezwa ili wananchi wengi wapate huduma ya umeme,” alisema Mgalu
Aliongeza kuwa, wakandarasi hao wanapaswa kuwa na mipango mbalimbali ya utekelezaji wa kazi kulingana na hali ya hewa ya maeneo wanayofanyia kazi ili kuweza kusambaza umeme katika vijiji vyote walivyopangiwa na Serikali ifikapo Juni 2019. Awali, Mkuu Wilaya ya Makete, Veronica Kessy, alimweleza Naibu Waziri kuwa, jumla ya vijiji 29 vimepangwa kuunganishiwa umeme kupitia mradi wa REA III mzunguko wa kwanza ambapo mkandarasi anaendelea na kazi ya usambazaji umeme vijijini, ingawa uongozi wa Wilaya hiyo umekuwa na wasiwasi na kasi yake katika usambazaji umeme.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akikata utepe ikiwa ni ishara ya wananchi katika Kijiji cha Bulongwa wilayani Makete kuanza kupata huduma ya umeme. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Makete, Veronica Kessy.
Baadhi ya nguzo za umeme zilizosimamishwa katika Kijiji cha Usungilo wilayani Makete mkoani Njombe ambapo kijiji hicho kitapata umeme kupitia mradi wa usambazaji umeme wa Awamu ya Tatu mzunguko wa kwanza.
Wananchi katika Kijiji cha Usungilo wilayani Makete, wakimsikiliza NaibuWaziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) wakati alipofika kijiji hapo kukagua kazi ya usambazaji umeme.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...