Na Ahmed Mahmoud, Arusha
Mkoa wa Arusha unakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na kituo cha mabasi chenye hadhi ya kisasa,kwani kilichopo sasa kinakabiliwa na ufinyu hali iliyoilazimu Halmashauri ya Jiji la Arusha kuja na mkakati wa kujenga kituo kikubwa cha mabasi chenye hadhi ya Kimataifa,kinachotarajiwa kujengwa katika Kata ya Olasiti iliyopo nje kidogo ya jiji hilo .
Hayo yamebainika wakati wa ziara ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alipotembelea Eneo litakapojengwa Kituo hicho ambapo amewataka viongozi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha kuwa kila mwananchi aliepisha eneo lake kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho analipwa fidia inayokadiriwa ni ni zaidi ya shilingi bilioni 1.7.
Gambo amesema kuwa mkoa wa arusha hauna standi inayoendana na hadhi ya jiji hilo na kuweza kufanya tathmini upya ya eneo hilo ili kuanza mchakato wa kuwalipa wale wanaostahili ili kuondoa sintofahamu ya kuwalipa watu wasio husika hali ambayoimekuwa ikisababisha malalamiko na migogoro mingi isiyo na tija kati ya wananchi na serikali yao.
“Hakikisheni mnapitia upya mchakato wa kuwalipa wananchi na ikiwezekana kila moja asimame kwenye eneo lake ili kuhakikisha mnamlipa mtu anayestahili kulipwa na sivinginevyo ili kuepusha migogoro isiyo na tija kati ya serikali na wananchi”alisisitiza mkuu huyo wa mkoa.
Viongozi wa mkoa wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo walipotembelea eneo litakapojengwa Kituo kikuu cha mabasi mkoani hapa eneo la Olasiti nje kidogo ya jiji la Arusha (Picha na a Ahmed Mahmoud Arusha)
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...