jumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kutumia fedha za ndani zaidi kwenye shughuli za kimaendeleo kuliko kutegemea misaada.

Mhe. Samia ameyasema hayo leo mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Pwani kwenye ukumbi wa Halmashauri ya mji wa Kibaha.Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alijitambulisha rasmi kama mlezi wa CCM mkoa wa Pwani na kuahidi kutoa ushirikiano wa kutosha .

Akizungumza na Wajumbe hao Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa Chama mkoani hapo kuhakikisha mali zote za Chama zinaleta tija kwa Chama.“Sasa ni wakati umefika kuangalia mali zetu ndani ya Chama labda Wilaya ilikuwa inamiliki vitu gani? Viwanja vya kujenga nyumba au vya michezo mali zozote ni kuziweka vizuri na kuhakikisha zinazalisha kwa manufaa ya Chama.”

Mhe. Samia amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi kimejipanga kutoa mafunzo ya Uongozi katika ngazi mbali mbali ambapo yeye binafsi amepangiwa mkoa wa Dar es Salaam, Pwani na Morogoro ambapo atashirikiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndugu Rodrick Mpogolo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mbunge  wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe. Silvestry Francis Koka pamoja na Viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Pwani mara baada ya kuwasili kwenye hafla fupi ya utambulisho kama Mlezi wa Chama hicho mkoa wa Pwani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa UVCCM Kibaha mjini Bi. Azilongwa Bohari pamoja na Viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Pwani mara baada ya kuwasili kwenye hafla fupi ya utambulisho kama Mlezi wa Chama hicho mkoa wa Pwani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Ndugu Ramadhani Maneno (kulia) akimtambulisha Mlezi wa CCM mkoa huo Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Pwani, kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo Mhandisi Evarist Ndikilo.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, Taifa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wajumbe wa kamati ya Siasa ya Mkoa wa Pwani mara baada ya kujitambulisha rasmi kama Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Pwani, hafla hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya mji Kibaha.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, Taifa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya Siasa ya Mkoa wa Pwani mara baada ya kujitambulisha rasmi kama Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Pwani, hafla hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya mji Kibaha.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...