Na Dotto Mwaibale, Kisarawe

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Suleiman Jafo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya uzinduzi wa Jukwaa la Kilimo utakaofanyika Kata ya Kurui wilayani Kisarawe mkoani Pwani.

Katika uzinduzi huo Waziri Jafo ambaye ni kiongozi wa juu wa serikali katika wilaya hiyo atakabidhi hati miliki za kimila za ardhi 315 ambazo zimeandaliwa na Shirika la The Winamwanga Cultural Heritage Association (TWCHA) katika maeneo ya vijiji vya Mafizi, Gwata, Kidugalo, Mtakayo, Zegero na Marui.

Akizungumza katika mkutano wa madiwani na wadau wa maendeleo ya kilimo wakati akitoa taarifa ya kazi zilizofanywa na shirika hilo kwa mwezi Novemba na Desemba 2017 Mratibu wa Mradi wa Kilimo kutoka Taasisi hiyo, Saidi Simkonda alisema waliona ni busara Waziri Jafo awe mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo kwa kuzingatia kuwa yeye ni mwenyeji wa eneo hilo.

"Tayari mchakato wa kumuomba Waziri Jafo kuwa mgeni rasmi tumeufanya tunachosubiri ni majibu yake kwani tunapenda kufanya tukio hilo mwanzoni mwa mwezi wa kwanza mwaka 2019" alisema Simkonda.Alisema mpaka sasa wana wanachama 750 kati ya hao 250 ni walemavu ambao wanamashamba katika kata hizo ambayo yanafanyiwa mchakato wa kupata hati miliki za kimila za ardhi huku 315 zikiwa tayari. 
Ofisa Ardhi wa Shirika la The Winamwanga Cultural Heritage Association (TWCHA) , Ivy Mwansepe, akimkabidhi taarifa ya kazi ya shirika hilo ya mwezi Novemba na Desemba mwaka 2017, Mgeni rasmi, Ofisa Kilimo wa Kata ya Kurui, Baraka Budangi, wakati wa mkutano wa Madiwani na wadau wa kilimo uliofanyika juzi wilayani Kisarawe mkoani Pwani juzi. Kulia ni Mratibu wa kilimo wa shirika hilo, Saidi Simkonda.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Zegero, Abdallah Binda akifungua mkutano huo.
Mkazi wa Kijiji cha Zegero Marcelina Mziray, akichangia jambo kwenye mkutano huo. Kutoka kulia ni Zulfa Tarazo na Mwenyekiti wa Kikundi cha Wakulima wa Kijiji cha Zegero, Fatuma Ali.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...