Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeutaka upande wa mashtaka kuhakikisha kuwa upelelezi katika kesi inayomkabili msanii wa Filamu nchini, Wema Sepetu, unakamilika kwa wakati, ili kesi iweze kuendelea.
Uamuzi huo umetolewa leo, Januari 28, 2019 na Hakimu Mkazi, Maira Kasonde, wakati kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa na upande wa mashtaka kudai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.
"Nataka upande wa mashtaka mkamilishe kwa wakati upelelezi ili kesi iweze kuendelea, kwa sababu ni kesi ya muda mrefu tangu ilipofunguliwa Mahakamani hapa Novemba mwaka jana na mpaka sasa upelelezi bado, ?" Alihoji.
Hakimu Kasonde ameaihirisha kesi hiyo hadi Februari 13, 2019 kesi hiyo itakapotajwa na kuwataka upande wa mashtaka kuhakikisha wanakamilisha upelelezi wao kwa wakati.
Wema ambaye ni Miss Tanzania 2006. alifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo Novemba Mosi, 2018, kujibu shtaka hilo la kuchapisha video ya ngono na kuisambaza kwenye mtandao ya kijamii.
Katika kesi ya msingi, Wema anadaiwa kuwa Oktoba 15, 2018 katika maeneo mbali mbali ya jiji la Dar es Salaam alichapisha video ya ngono na kusambaza katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...