Na Karama Kenyunko globu ya Jamii
OFISA Msaidizi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Kituo cha Gerezani Kariakoo, Dar es Salaam, Charles Kapongo amefikishwa katika Mahakama ya Wilayaya Ilala akikabiliwa na tuhuma za kupokea rushwa ya Sh. milioni 10.
Akisoma hati ya mashtaka wakili wa serikali kutoka Takukuru, Dumas Muganyizi amedai mbele ya Hakimu Mkazi, Flora Haule kuwa, Januari 25, mwaka huu katika maeneo ya ofisi za TRA zilizopo Gerezani Kariakoo ndani ya Wilaya ya Ilala, mshtakiwa alitenda kosa.

Imedaiwa siku hiyo mshtakiwa Kapongo akiwa mwajiriwa na TRA, alipokea rushwa ya USD ,4200 Ambazo ni Sawa na Sh. milioni 10, kutika kwa Naibu Magala ambaye ni mwajiriwa wa kampuni ya Ushauri ya Hakha Business Accounting.
Wakili Flora Anaendeleaje kudai kuwa, fedha hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kushawishi kupunguza makadirio ya kodi ya kampuni hiyo, kutoka Sh 45,571,664 kwenda Sh. milioni nane kitendo ambacho ni kinyume na maadili yake ya kazi.
Hata hivyo, mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na yuko nje kwa dhamana baada ya kufanikiwa kukamilisha masharti yaliyowekwa Na Mahakama ambapo alitakiwa kuwa na wadhamini kati yao mmoja atoke kwenye taasisi yoyote inayotambulika Na wote wametakiwa kusaini bondi ya Sh. Milioni tano.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi bado haujakamilika na kesi hiyo itatajwa Februari 11.2019
FISA
Msaidizi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Kituo cha Gerezani
Kariakoo, Dar es Salaam, Charles Kapongo akifishwa katika Mahakama
ya Wilayaya Ilala akikabiliwa na tuhuma za kupokea rushwa ya Sh. milioni
10.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...