*Ni wakati tukio la utiwaji saini wa mkataba wa ushirikiano kati ya TFS na NLUPC


Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

WAKATI mjadala ukiendelea kuhusu tukio la bundi kutua Bungeni, leo hii katika tukio la utiwaji saini wa mkataba wa ushirikiano kati ya Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) na Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi(NLUPC) Paka a.k.a Nyau ameingia katika ukumbi wa mikutano wa Mpingo House jijini Dar es Salaam.

Paka huyo aliingia ukumbini hapo saa sita kasoro dakika tano ikiwa ni dakika chache kabla ya tukio la utiwaji saini kufanyika ambapo haijulikani alitokea wapi.Wakati anaingia ukimbini Paka huyo alianza kupiga kelele za milio ule maaruf wa Nyauuuu...nyau...nyau... kwa staili yao kama ambavyo tumezoea kuusikia masikioni.

Baada ya kuingia ukumbini hakuwa na makeke kwani baada kufika alikwenda kukaa pembeni ya ukutano na kisha akajituliza tuli.

Baadhi ya waandishi waliokuwa ukumbini hapo walijikuta wakianza kucheka kutokana na Paka huyo kuingia.Kwa kuwa hakuna na vurugu yoyote kilichobaki ikawa ni kumuangalia na kwa huu ni ulimwengu wa teknolojia ,kilichofuata ikawa ni kumpiga picha(kama unavyoona hapo pichani).

Hata hivyo baadhi ya waandishi waliamua kumfuata ili kumuondoa mahali alipo lakini aligoma kuondoka.Wakati Paka huyo akiwa mkutanoni hapo waliokuwa meza kuu na wale wa viti vilivyokuwabna baadae akaamua kusogea.

Hivyo wakati wa utiwaji saini mkataba huo aliondoka ukumbini na baada ya tukio kukamilika akarejea tena.

Ujio wake kwa mara ya pili ulisababisha baadhi ya waandishi kujiuliza na maswali kuhusu Paka huyo ambapo baadhi yao wakajikuta wakizungumzia tukioa Bundi kutua Bungeni ambapo Spika wa Bunge Job Ndugai aliamua kuelezea tukio hilo na kwamba kwa Dodoma Bundi wa usiku ndio mwenye madhara na si bundi anayeonekana mchana.

Haifahamiki Paka aliyeingia ukumbi wa mikutano wa Mpingo House leo alikuwa na mkakati gani.Hiyo itabaki kuwa siri ya Paka mwenyewe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...