WAFANYABIASHARA watano wa jijini Dar ea Salaam wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashitaka manne ya kuingiza kemikali bila kuwa na kibali cha Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA).

Akisoma hati ya mashtaka, wakili wa serikali, Wankyo Simon amewataja wfanyabiashara hao kuwa ni Jumanne Mazunde, Godfrey Kiwelu, Nsia Mbonika, Chanikan Mhina na Joseph Omoll.
Wakisomewa mashtaka yao leo Februari 26.2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, imedaiwa,  Septemba 13, 2017 huko katika maeneo ya Ubungo Maziwa Dar es Salaam, mshtakiwa Mazunde aliingiza kemikali mbalimbali zenye uzito wa kilogramu 1,514.5 kutoka Nairobi nchini Kenya bila kibali cha mkemia.

Pia mashitakiwa, Godfrey na Mbonika wanadaiwa Septemba 13, 2017 maeneo ya Ubungo Dar es Salaam, waliingiza kemikali zenye uzito wa kilogramu 87,  zilizoingizwa kutoka Nairobi nchini Kenya bila kibali cha mkemia. Imeendela kudaiwa kuwa, siku na mahali hapo mshtakiwa, Mhina aliingiza kemikali zenye uzito wa kilogramu 100 bila kuwa na kibali cha mkemia.

Katika shitaka la nne, Septemba 13, 2017 maeneo ya Ubungo washtakiwa wote waliingiza kemikali bila kuwa na kibali. Hata hivyo, washitakiwa  wamekana mashitaka hayo na kwa mujibu wa upande wa mashitaka upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Akiwasomea msharti ya dhamana, Hakimu Shaidi amewataka washitakiwa kuwa na wadhamini wawili kutoka serikalini na vitambulisho watakaosaini kulipa Sh milioni 10. Hata hivyo, washitakiwa watatu walipata dhamana huku wawili walirudishwa rumande kwa kukosa dhamana. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 12 mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...