Mwandishi wa kituo cha Habari cha ITV na Readio One Mkoani Kagera Bw. Audax Mtiganzi amefikishwa katika mahakama ya mwanzo Wilayani  Bukoba mapema Machi 20, 2019, kwa kosa la kushambulia na kudhuru mwili. 
Akisomewa maelezo ya kosa,hakimu wa mahakama hiyo Owemilembe Ishabakaki amesema, mshitakiwa alitenda kosa hilo katika mtaa wa Kashenye (anapoishi) Januari 21,2019 saa tatu usiku.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 255/2019 Mtuhumiwa kwa kumpiga na kumdhuru  bila halali mlalamikaji Bw. Phinias Bashaya Mwandishi Wa Habari Wa Mwananchi Communications Ltd, Mkoa Wa Kagera.

Baada ya kusomewa shitaka mlalamikaji alihoji kutokuwepo kwa shitaka la kuharibu mali, na madai ya mshitakiwa kuwa mlalamikaji alijaribu kumpa sumu na mahakama imeagiza hati ya mashitaka ibadilishwe.

Mtuhumiwa huyo yupo nje kwa dhamana, baada ya kukamilisha masharti ya dhamana ambapo mdhamini amesaini bondi ya shilingi laki mbili na kesi itatajwa tena March 25 mwaka huu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...