Naibu Waziri Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (watatu kulia) akiwasili
katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Katoliki Ruaha (RUCU) jana na
kupokewa na vijana wanaoshiriki mashindano ya Kabati Star Search ambapo
mashindano hayo yanafanyika hapo, watatu kushoto ni Ritha Kabati
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Iringa ambaye ndiye mwandaaji wa
mashindano hayo.
Naibu Waziri Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (wapili
kushoto)akisalimiana na mchekeshaji maarufu Baraka Mwakipesile
anayeigiza kama Rais Magufuli ambapo kwa sasa anajulikana kama Baraka
Magufuli mara baada ya uzinduzi wa mashindano ya Kabati Star Search
yaliyofanyika jana Mkoani Iringa, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya Mufundi Bw.Netho Ndilito.
Mmoja ya washiriki wa mashindano
ya Kabati Star Search Yahya Hamadi kutoka Kata ya Mwangata Mkoani
Iringa akionyesha uwezo wake kwa kuimba wimbo wa Msanii Young Killer
katika mashindano hayo yaliyofanyika jana ambapo yalizinduliwa na Naibu
Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza
(hayupo pichani).
Mmoja ya washiriki wa mashindano
ya Kabati Star Search Sophia Kalinga kutoka Kata ya Gangilonga Mkoani
Iringa akionyesha uwezo wake kwa kuimba wimbo wa You Raise Me Up
kutoka kwa msanii Josh Groban katika mashindano hayo yaliyofanyika jana
Mkoani hapo.
Naibu Waziri Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (watatu kushoto ) akiwa
katika picha ya pamoja na Majaji wa Shindano la Kabati Star Search mara
baada ya uzinduzi wa shindano hilo lililofanyika jana Mkoani Iringa,
wapili kushoto ni muandaaji wa shindano hilo Ritha Kabati Mbunge wa Viti
Maalum (CCM) Mkoa wa Iringa .
Msanii wa Mkoa wa Iringa Ezra
Msiliova maarufu kama Eze Nice akiimba kwa hisia wimbo wa kuisifia
Tanzania mbele ya Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Mhe.Juliana Shonza wakati wa uzinduzi wa Shindano la Kabati Star
Search lilofanyika jana Mkoani Iringa.
………………………………………………………………………………
Na Anitha Jonas- Iringa
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza ameto wito kwa wadau mbalimbali
nchini kujitokeza kuandaa Mashindano ya kusaka vipaji vya Muziki kwa
vijana kwa kuanzia ngazi za Mikoa na Wilaya.
Mheshimiwa Shonza ametoa wito huo
jana Mkoani Iringa alipokuwa akizindua Tamasha la Ritha Kabati Star
Search lililolenga kusaka vipaji vya vijana wanaojua kuimba muziki na
tamasha hilo limekusanya vijana zaidi ya 150 kutoka maeneo mbalimbali ya
wa Mkoa wa Iringa.
“Ninapenda kumpongeza Mhe.Ritha
Kabati Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa kwa kuandaa Tamasha lenye
tija kwa taifa kama hili, pia ninaomba wadau mbalimbali wenye uwezo
kuandaa matamasha kama haya kwa kuanzia ngazi za mbalimbali ndani ya
mikoa na wilaya zetu kwa ndiko waliko vijana wenye vipaji, tuwasaidie
kufikia ndoto zao kwa manufaa ya taifa,”alisema Mhe.Shonza.
Akiendelea kuzungumza katika
uzinduzi huo wa Kabati Star Search Naibu Waziri huyo alimtaka Afisa
Utamaduni wa Mkoa wa Iringa kuandika barua kwa Baraza la Sanaa la Taifa
(BASATA) ya kuomba wataalamu kuja kutoa mafunzo kwa wasanii chipukizi wa
muziki wa mkoa huo kwa lengo la kuwa ongezea maarifa wasanii hao.
Naye muandaaji wa Tamasha hilo
Mhe.Ritha Kabati alieleza kuwa amekuwa akiwaona vijana wa mkoa huo na
kuwa wanavipaji ila wamekuwa wakikosa jukwaa la kuonyesha vipaji vyao
na ndiyo maana aliamua kuanzisha mashindano hayo ambayo yatawainua
vijana wa mkoa wa Iringa nao kuanza kusikika Kitaifa na Kimataifa kama
wasanii wengine maarufu hapa nchini.
“Katika kuhakikisha mashindano
haya yanaleta mafanikio nilizungumza na mmoja wa walezi wasanii wa
Muziki nchini Bw. Said Fella Maarufu kama Mkubwa Fella kuhusu
kuwasaidia washindi wa mashindano haya na tukakubaliana kuwa mshindi wa
kwanza mpaka watatu atawachukua na kwenda kuwafunza vizuri kisha
watarekodi nyimbo zao na pia wataimba na wasanii maarufu hapa nchini na
atahakikisha na hizo nyimbo zao zinapigwa katika vituo vya redio na
televisheni mbalimbali nchini,”alisema Kabati.
Pamoja na hayo Kabati alieleza
kuwa vijana wa Iringa wamesema wanataka nao Mkoa wao uonyesha kuwa
unavipaji vyenye uwezo mkubwa wakufikia ngazi za Kimataifa kwani
kupitia mashindano ya mpira wa miguu ya Kabati Challenge Cup vijana
watatu tayari wamechukuliwa na timu za mpira za Afrika Kusini kwa lengo
la kwenda kuchezea timu za vijana na watakuwa wanasomeshwa huko pia .
Halikadhalika na mmoja wa
washiriki wa mashindano hayo Yahya Hamadi alimshukuru mbunge huyo wa
viti maalum kwa kuandaa mashindano hayo na ameahidi kuwa atajitahidi
kufanya vizuri kwani anaamini kupitia jukwaa hilo nae anaweza kuja
kuwa msanii maarufu katika Taifa.
Hata hivyo Naibu Waziri Shonza
aliwasihi majaji wa mashindano hayo kutenda haki katika maamuzi
wanayoyafanya kwani wao ndiyo wenye dhamana ya kutoa msanii
atakayetangaza mkoa na taifa kwa ujumla katika ngazi za Kimataifa,ambapo
mmoja wa majaji hao Bw.Roger Magoha kwa niaba ya wenzake aliahidi
kusimamia hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...