Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

FORUM CC kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya wameamua kuwatanisha wadau kutoka mashirika mbalimbali kwa lengo la kuwa na jukwaa ambalo litatumika kujadili masuala yanayohusu hali ya mabadiliko ya tabianchi.

Pamoja na mambo mengine Forum CC na mashirika hayo wamejadili kwa kina namna bora ya kufanya kazi kwa karibu na mamlaka za Serikali kwa lengo la kuhakikisha jamii ya Watanzania inakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu mabadiliko ya tabia nchi ambayo athari zake zinagusa kila mahali.

Akizungumza leo Mei 9, 2019 wakati majadiliano hayo yaliyofanyika Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Forum CC Rebecca Muna amefafanua wao kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya wameamua kuwakutanisha wadau hao waliopo kwenye mashirika na asasi za kiraia kujadili kwa kina namna bora ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

"Sababu iliyotufanya tukutane hapa leo tunataka tuwe na ushirikiano wa karibu na Serikali.Tunataka kufanya kazi na viongozi, hivyo wadau wote wa maendeleo tutakuwa na jukwaa litakalotupa fursa ya kufanya kazi kwa pamoja hasa za kutatua changamoto za athari za tabianchi,"amesema Muna.

Amefafanua hali ya mabadiliko ya tabianchi yamesababisha nchi kuwa na ukame, mafuriko, kina cha bahari kuongezeka, kupanda kwa joto na magonjwa ya mazao , hivyo kusababisha madhara ya aina mbalimbali kwa jamii.

Amesisitiza kupitia jukwaa la majadiliano ambalo litaanzishwa na wadau maana yake watakuwa na eneo maalumu ambalo litawakutanisha na kujadili kwa kina hali ya mabadiliko ya tabianchi.

"Lengo letu ni kuwa na jukwaa la pamoja ambalo hilo litatuwezesha sote kwa umoja wetu kupata fursa ya kujadili na kupata ufumbuzi wa namna sahihi ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi,"amesema Muna.

Hata hivyo amesema umefika wakati wa kuwepo kwa mfumo sahihi ambao utawawezesha mashirika, asasi za kiraia na wadau wa maendeleo kushirikishwa kikamilifu na Serikali katika kuleta maendeleo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Forum CC Euster Kibona amesema kuwa pamoja na kuweka mikakati ya kujadili kuhusua mabadiliko ya tabianchi wamekumbusha kuhusu uwajibika ambapo kupitia mada yake iliyohusu dhana ya uwajibika alifafanua kwa kina huku akisisitiza uwajibikaji ni ushirikiano baina ya pande mbili.

"Uwajibikaji ni muhimu katika kufuatilia masuala mbalimbali ya kimaendeleo na hata hili la mabadiliko ya tabianchi nalo lazima tujadiliane kuhusu namna bora ya kuwajibika kwani eneo hilo limekuwa na changamoto kubwa.

"Katika kuwajibika lazima ufahamu nani anawajibika katika lipi na anawajibika kwani.Hata hivyo ili kufanikiwa ni jambo linalohusu uhusiano wa zaidi ya mtu mmoja.Hivyo ni wakati wetu kuweka mikakati ya namna bora itakayowezesha kila mmoja kwa nafasi yake kuwajibika,"amesema Kibona. 

Awali Ofisa Programu,Ushawishi na Utetezi kutoka TGNP Deogratius Temba amesema mabadiliko ya tabianchi yanagusa maeneo mbalimbali yakiwemo ya jinsia na athari zake zinakwenda moja kwa moja kwa mtoto wa kike.

"Athari za mabadiliko ya tabianchi ni nyingi ikiwemo ya ukame ambayo inasababisha hata maeneo ambayo wananchi walikuwa wanateka maji yakauka na kusababisha wanawake kuanza kufuata maji umbali mrefu na hivyo kusababisha hata matukio ya ukatili wa kijinsi.

"Hivyo eneo hili linagusa maeneo mengi na hivyo kila mmoja wa nafasi yake anayo nafasi ya kujadili na kuweka mipango na hasa ambayo inatokana na maoni ya wananchi katika maeneo husika.

"TGNP tumekuwa tukishirikiana na wananchi kuibua ajenda na kisha wananchi kuzipeleka katika mamlaka husika na hivyo hata haya masuala ya tabianchi ni vema wananchi wakajengewa uwezo ili kuwa na uelewa,"amesema Temba

Mwenyekiti wa Bodi ya Forum CC Euster Kibona akizungumza jambo wakati wa kikao cha mashirika ya kirai kujadili hali ya mabadiliko ya tabianchi na mchango wa mashirika hayo katika kutafuta ufumbuzi wake kwa kushirikiana na Serikali.
Mkurugenzi Mkuu wa Forum CC akizungumza na wadau wa maendeleo kupitia mashirika ya kiraia ambauo yamekutana kujadili namna bora ya kujadili changamoto za mabadiliko ya tabia nchi kwa kushirikiana na vongozi wa serikali.

Ofisa Programu,Ushawishi na Utetezi kutoka TGNP Deogratius Temba akifafanua jambo kuhusu mabadiliko ya tabianchi yanavyoarithi moja kwa moja masuala ya kijinsia nchini Tanzania wakati wa kikao kati ya Forum CC na mashirika ya kiraia ambayo yamekutana kwa malengo mbalimbali likiwemo la kuwepo kwa jukwaa la pamoja na wadau hao

Sehemu ya washiriki wa mkutano uliondaliwa na Forum CC kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya wenye lengo la kuangalia namna bora ya mashirika ya kiraia kushirikiana na Serikali kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...