Na Said Mwishehe, Blogu ya jamii
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inamshikilia aliyewahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu kwa tuhuma za vitendo vinavyoashiria uwepo wa rushwa.
Nyalandu ambaye kwa sasa ni Kada wa Chadema amekamatwa leo saa tisa Alasiri mkoani Singida ambapo baada ya kukamatwa amechukuliwa na kwenda kuhojiwa na TAKUKURU.
Akizungumza na Michuzi Blog kwa njia ya simu jioni hii, Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU)Mkoa wa Singida Joshua Msuya amesema Nyalandu wamemkamata leo kutokana na kufanya vitendo vinavyoashiria uwepo wa rushwa.
"Ni kweli tumemkamata Nyalandu kwa ajili ya kufanya naye mahojiano, kuna mikutano ya kisiasa ambayo wanaifanya na kuna viashiria vya vitendo vya rushwa.Hivyo tumemkamata kwa ajili ya kumhoji.Tunaomba ifahamike tunamhoji kwasababu ya kuwepo viashiria vya vitendo vya rushwa na si kwamba tumemkamata akitoa rushwa,"amesema Msuya.
Alipoulizwa kama bado wanamshikilia au laa ,Msuya amejibu wao baada ya kumhoji wamemkabidhi kwa vyombo vingine vya ulinzi na usalama kwa mahojiano zaidi.
Taarifa za kwamba amevamiwa na watu wasiojulikana wakia na silaha, Joshua amejibu sio kweli kwani Nyalandu kabla ya kuchukuliwa kwa ajili ya kuhojiwa alipewa taarifa na hivyo alikuwa anajua kuwa anahitajika TAKUKURU.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...