NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
TANZANIA
na Zambia kupitia Mifuko ya Fidia kwa Wafanyakazi, wamesaini mkataba wa
ushirikiano utakaosaidia kubadilishana uzoefu kati ya mifuko hiyo.
Akizungumza
mara baada ya kutiliana saini mkataba huo, kwenye ofisi za WCF jijini
Dodoma Jumatatu Mei 27, 2019, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi (WCF), Bw. Masha Mshomba alisema, Zambia inauzoefu wa zaidi
ya miaka 40 katika sekta ya hifadhi ya jamii katika kulipa mafao ya
Fidia kwa Wfanyakazi kwa hivyo makubaliano hayo yana manufaa makubwa.
Alisema
makubaliano hayo ni ya kawaida kati ya mifuko na kwamba WCF na WCFCB
watabadilishana uzoefu katika masuala ya namna ya ulipaji mafao, namna
ya kuzuia ajali na magonjwa kazini kwa sababu mambo hayo ni muhimu sana
katika mifuko ya fidia.
“Nguvu
kazi ya taifa inapolindwa tija huongezeka makazini na jambo hili
hudhihirika pale pato la taifa linaongezeka hususan kwetu sisi ambao
tunajenga uchumi wa viwanda jambo hilo ni muhimu sana.”Alisema Bw.
Mshomba.
Alisema
kwa uzoefu ambao Zambia watakuwa wameupata kutoka kwao wataweza
kuboresha huduma zao, na tayari Dkt. Nkumbula amethibitisha kuwa
serikali ya Zambia inautegemea Mfuko huo katika kusaidia nguvu kazi ya
taifa.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi Zambia (WCFCB), Dkt. Elizabeth Lungu Nkumbula alisema,
imekuwa ni siku njema kwao kwa kujenga ushirikiano wa pamoja katika eneo
la hifadhi ya jamii.
“Zambai
na Tanzania chini ya uongozi wa Dkt. Keneth Kaunda na Mwalimu Nyerere,
waliweza kujenga reli ya TAZARA na bomba la mafuta TAZAMA kwa hivyo
ushirikiano huu wa leo ni kumbukumbu ya ushirikiano uliojengwa kwa muda
mrefu na viongozi hao wa mataifa hayo mawili.” Alifafanua.
Alsema
ushirikiano huu utasaidia pande mbili kubadilishana uzoefu katika kutoa
huduma za ulipaji fidia na mbinu za kuzuia majanga yatokanayo na kazi
na hivyo kusaidia mataifa hayo kukuza uchumi.


Bw. Masha Mshomba akisaini
Dkt. Elizabeth Lunhgu Nkumbula, akiweka saini yake.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Masha Mshomba
akizungumza kwenye hafla hiyo. Kulia ni mgeni wake, Dkt. Elizabeth Lungu
Nkumbulu.
Mwenyekiti
wa bodi ya wakurugenzi ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kutoka Zambia,
(WCFCB), Dkt. Elizabeth Lungu Nkumbula akizungumza katika hafla hiyo.
Bw. Mshomba akimkabidhi zawadi ya picha mgeni wake, Dkt. Elizabeth Lungu Nkumbula.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...