Na, Editha Edward-Tabora
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora Wamemtaka Mkurungezi wa Halmashauri hiyo kueleza ni vifungu gani vya walaka vya Tamisemi anavyotumia kusitisha posho za kujikimu za Madiwani
Yamesemwa hayo katika kikao cha madiwani kilichofanyika Wilayani Nzega Mkoani Tabora ambapo kikao hicho kimeudhuliwa na mmoja wa Wajumbe ambae ni Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini Mhe. Hamis Kigwangalla ambaye ameibua hoja hiyo kwa lengo la kujua sababu zinazo sababisha kwa Kutolipwa posho kwa muda wa Miezi Minne
"Madiwani wote wanalazimika kulala kila wanapokuja hapa kufanya kikao, Sisi Mazingira yetu halisi ni Vijijini hapa tumekuja tu kufanya kikao tunamtaka Mkurugenzi azingatie sheria ya Fedha ya Serikali za mtaa"Amesema Kigwangalla
Nae Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Msalika Robert akamtaka katibu Msaidizi anayeshughulikia Serikali za mitaa Vitaris Linuma kutoa ufafanuzi juu ya jambo hili
"Kila diwani Anatakiwa kulipwa posho ya usafiri Anatakiwa kulipwa posho ya kuhudhuria kikao na Fedha ya kujikimu ambayo Anatakiwa kulipwa pesa ya kulala"Amesema Linuma
Licha ya maelezo hayo mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Nzega Vijijini akamsimamisha Mkurungezi wa Halmashauri hiyo Seleman Sekeiti nae akatoa maelezo."Suala la kulipwa posho nalilejesha kwa Mwenyekiti wa baraza hili maamuzi mtakayoamua hapa ndiyo yatakayo kuwa maamuzi ya baraza "Amesema Sekeiti
Aidha kutokana na kupata tafasiri sahihi ya mkanganyiko huo Wajumbe wa baraza la Madiwani wa Nzega wote kwa kauli moja wameridhia na kurejeshwa kwa posho za kujikimu.
Pichani ni mbunge wa Nzega vijijini Mhe. Hamis Kigwangalla akizungumza jambo katika kikao cha madiwani.
Pichani ni madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Nzega Mkoani Tabora wakiwa katika kikao kilichofanyika mjini Nzega.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...