Anaandika Abdullatif Yunus wa Michuzi TV.
Mkoa wa Kagera umeendelea kung'ara katika ramani ya kiuchumi na uwekezaji baada ya kuzindua rasmi Soko Kuu la madini ya Tin yanayopatikana Wilayani Kyerwa Mkoani Kagera pekee, Huku wachimbaji hao wakitakiwa kuwa wazalendo kwa kuhakikisha wanalitumia soko hilo kujinufaisha wao pamoja na Taifa, na kuacha kabisa Biashara ya magendo ambayo ilikuwa ikifanyika kwa kuyatorosha madini hayo na kuyauza Nchi jirani kwa njia zisizo kuwa harali.
Akizungumza na Wananchi, wachimbaji na Viongozi mbalimbali waliohudhuria katika shughuli hiyo ya Uzinduzi wa Soko kuu la Madini Wilayani Kyerwa, Naibu Waziri wa Madini Mh. Stanslaus H. Nyongo amesema ili soko hilo la madini liwe na Tija na kuvutia Wafanyabiashara ni lazima kuwa na wachimbaji walioombea Leseni hivyo wale wote ambao watakuwa wanamiliki Leseni za uchimbaji lakini wameshindwa kuziendeleza wanyanganywe mara moja, na huku akitoa maelekezo kwa afsa madini Mkoa kama kuna mtu binafsi, au kampuni iliyoshindwa kuendeleza leseni yake na wakati tayari lipo soko la uhakika, ndani ya Mwezi mmoja apatiwe hati ya makosa na afutiwe leseni yake, na leseni hiyo wapewe walio tayari.
Awali Akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa yanapopatikana madini hayo Mh. Rashid Mwaimu ameendelea kutahadharisha wale wote waliokuwa wakifanya shughuli za magendo ya madini hayo kuwa, Serikali ipo macho na itaendelea kuelekeza nguvu zake zote katika sekta hiyo, ili kuhakikisha madini hayatoroshwi tena na huku akitoa rai kwa Taasisi zote zinazotoa huduma katika mnyororo wa thamani wa madini, kuweka mazingira rafiki ili kuvutia wafanyabiashara ambao wataanza kufika Sokoni hapo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti amesema lengo la Mkoa wa Kagera ni Kuifanya Biasahara ya rasilimali Madini ya Tin, kufanya vizuri zaidi katika Soko la Dunia kwa kuanzia kuboresha mazingira kwa wachimbaji wadogo, kupitia kutatua changamoto zao zilizopo kwa sasa ikiwemo changamoto ya mitaji na umeme mgodini, ili uzalisahaji wa madini kuongezeka kulingana na Takwimu zilivyo kwa sasa, na kutoa wito kwa wawekezaji wakubwa Kufika Mkoani Kagera kuwekeza katika rasilimali hii yenye faida kubwa katika uzalishaji.
Madini ya Tini yamekuwa muhimu kupitia matumizi yake mbali mbali yakiwemo,Kutengenezea vifungashio vya chakula na vinywaji, rangi aina zote, risasi, vioo, magari, simu za mikononi, Kompyuta, Reli, vifaa vya Kijeshi n.k.
Pichani Ni Meneja kutoka Kiwanda cha Uchenjuaji Tin (Tanzaplus) Ndg. Maarufu akitoa maelezo kwa Viongozi juu ya Namna madini hayo yanavyoandaliwa.
Pichani ni Naibu Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyongo akifurahia moja ya madini ya Tin ambayo yameshayeyushwa tayari kwa matumizi mbalimbali.
Pichani ni Afsa madini Mkoa wa Kagera, Mhandisi Lucas M. Akisoma risala kwa mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa soko kuu la madini ya Tin Kyerwa, Kagera.
Pichani Naibu Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyongo akislimia na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Kyerwa Ndg. Mhagama, mapema Mara baada ya kuwasili Wilayani humo tayari kwa Uzinduzi wa Soko la Madini.
Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akitoa salaam zake kwa Wananchi (hawapo pichani) katika shughuli ya Uzinduzi wa Soko la Madini aina ya Tin Wilayani Kyerwa.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Madini Mh. Stanslaus Nyongo akihutubia Wananchi, viongozi na wachimbaji wadogo wadogo (hawapo pichani) katika Uzinduzi wa Soko Kuu la Madini ya Tin Wilayani Kyerwa Mkoani Kagera.
Pichani kushoto Ni Naibu Waziri wa Madini Mh. Nyongo, Mbunge wa Kyerwa Mh. Bilakwate, Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mh. Mwaimu, Mkuu wa Mkoa Kagera Mh. Gaguti na Katibu Tawala Mkoa Kagera Profesa Kamuzora wakisaidiana kuzindua kufunua jiwe kama Ishara ya Uzinduzi rasmi wa Soko la Madini ya Tin Kyerwa.
Pichani Viongozi wakiwa wamebeba Tin iliyoyeyushwa kama ishara ya Uzinduzi wa Soko Kuu la Madini ya Tin.
Jiwe la Uzinduzi kama linavyoonekana pichani.
Pichani ni Tin ikiwa tayari imeyeyushwa ikisubiri matumizi mengine mbambali, na kila pande moja lina zaidi ya kilo 50, ambapo kila kilo moja huuzwa zaidi ya shilingi elfu kumi na tano.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...