Mwenyekiti
wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk Jones Kilimbe
(kushoto) akipongezwa na Mjumbe wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Derek
Murusuri, baada ya kumalizika kwa hafla ya kuzindua Mkataba wa Huduma
kwa Mteja (Client Service Charter) wa Mamlaka hiyo jijini Dodoma leo.
Akizindua
Mkataba huo, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Eng. Isack
Kamwelwe (hayuko pichani), ameipongeza Bodi na Menejimenti ya TCRA kwa
kuwa mfano bora kwa taasisi nyingine za umma kuandaa Mkataba wenye lengo
last kuboresha huduma.
Waziri
Kamwelwe amempongeza Mkurugenzi mkuu wa TCRA, Eng. James Kilaba
(katikati) kwa ubunifu na umakini mkubwa katika kufanikisha uandaaji wa
mkataba huo utakaowafanya watanzania wajivunie huduma bora na kujaliwa
katika taifa lao.
Waziri
Kamwelwe amesema kuwa uboreshaji wa huduma za Mawasiliano nchini pia
utasaidia kuondoa rushwa kabisa kwani katika e-government, mteja
atahudumiwa pasipo kuonana na mtoa huduma uso kwa uso.
"Ni katika kuonana uso kwa uso vitendo vya rushwa vinafanyika, katika simu ukioomba rushwa utamulikwa tu," alisema.Tanzania chini ya Rais Magufuli, inapigiwa mfano katika bara la Afrika kwenye vita dhidi ya rushwa.
Akiongea
katika hafla hiyo kubwa iliyofanyika katika ukumbi ya Jakaya Kikwete,
jijini Dodoma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe George Mkuchika, amezitaka taasisi nyingine
zote za umma kuiga mfano wa TCRA na kuandaa mikataba ya wateja.
Ameitaka
Mamlaka hiyo kuutekeleza Mkataba huo ili kusaidia kuharakisha maendeleo
ya kijamii na kiuchumi nchini, hasa ukizingatia unyeti wa sekta ya
Mawasiliano.
Naye
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza,
mbali na kuipongeza TCRA kwa kazi nzuri ya kuwahudumia watanzania,
ameishukuru Mamlaka kwa mahusiano mazuri ya kikazi baina yao.
Hafla
hiyo imehudhuriwa viongozi mbalimbali wakiwemo Naibu Waziri wa Ujenzi,
Mawasiliano na Uchukuzi, Eng. Atashasta Nditiye na Naibu mwingine katika
Wizara hiyo, anayeshughulikia sekta ya Ujenzi, Eng. Elias Kuandikwa.
Wengine
ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Eng. Mary
Sassabo, Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo, Dk Jim Yonazi pamoja na
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi ambaye alimwakilisha Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...