Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ameupongeza uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) kwa kutenga sh. bilioni moja kwa ajili ya kuwawezesha wanataaluma kufanya tafiti zaidi hasa zinazogusa matatizo ya jamii moja kwa moja.

Waziri Ndalichako ametoa pongezi hizo jijini Dar es Salaam wakati akifunga maadhimisho ya tano ya Wiki ya Utafiti ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo amesema tafiti ni muhimu katika kuleta maendeleo kwa kujenga na kukuza uchumi wa viwanda nchini.

Prof. Nalochako amesema serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kujenga uchumi wa viwanda lengo likiwa kuhakikisha kunakuwa na viwanda ambavyo vinatumika kuzalisha bidhaa na kutoa huduma zitakazotosheleza jamii ya Kitanzania na kusaidia kuongeza ajira kwa vijana.

Akizungumzia Wiki ya Utafiti Waziri Ndalichako amesema inawapa wadau wa utafiti na ubunifu jukwaa la kufahamu shughuli za utafiti zinazofanyika; sehemu gani kuna mapengo na changamoto; na mikakati gani ya kimipango inahitajika ili kuziba mapengo pamoja na kutatua changamoto zilizobainika.

"kama taifa, tuna wajibu mkubwa na fursa nyingi za kuweza kutumia utafiti, ubunifu na ujasiriamali hususan kupitia sekta ya elimu ili kuongeza kasi ya maendeleo ya viwanda nchini. Kufanya hivyo, kutawezesha kutekeleza azma ya Serikali ya awamu ya tano ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Dira ya Taifa ya 2015, ya kuhakikisha kuwa Tanzania inafikia uchumi wa kati kupitia viwanda." Amesisitiza Waziri Ndalichako.

Nae Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa William Anangisye amesema kuwa tafiti zinazofanyika zinafanya Chuo kuweza kutambulika kimataifa.

Amesema wanataraji kutenga sh.bilioni moja kwa ajili ya kazi za utafiti ili kuweza matokeo katika maendeleo katika utengenezaji sera mbalimbali.
Makamu Mkuu wa Chuo hicho amesema kuwa tafiti ndizo kiungo na serikali katika kusaidia wananchi kutatua changamoto mbalimbali.

 Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akipata maelezo katika maonesho ya Utafiti katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akifunga wiki ya Tano ya Utafiti wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) uliofanyika katika ukumbi wa Nkrumah wa Chuo hicho.
 Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam -Profesa William Anangisye akitoa maelezo kuhusiana na Wiki ya Tano ya Utafiti wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
 

 Baadhi ya wadau katika wiki ya Tano ya Utafiti wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...