Na Humphrey Shao, Michuzi Blog
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la usimamizi wa Mazingira NEMC, DK.Samuel Gwamaka amezungumza na Waombolezaji walikusanyika nyumbani kwa marehemu na kutaja mchango wake katika uhifadhi wa mazingira nchini
Akizungumza na vyombo vya habari na waombolezaji Nyumbani kwa marehemu kinondoni Dar es Salaam,Dr Gwamaka ametaja namna Marehemu alivyoshiriki katika uanzishwaji wa baraz ala Mazingira nchini.
"Dr. Mengi ndio alikuwa Mwenyekiti wa kwanza wa baraza na aliyeshiriki kuunda baraza na sheria yake ambayo imeleta mabadiliko makubwa ya uhifadhi wa mazingira nchini kulinganisha na uko nyuma.
Ametaja kuwa Dk. Mengi amedumu katika nafasi hiyo kwa miaka kumi ambayo ndio wakati baraza liliweza kuimarika sana na kujilikana kila mahali hivyo tunatambua mchango wako mkubwa katika uhifadhi wa Mazingira.
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la usimamizi wa Mazingira NEMC, DK.Samuel Gwamaka akizungumza mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo wa msiba wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Marehemu Dr Reginald Mengi
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la usimamizi wa Mazingira NEMC, DK.Samuel Gwamaka akisaini kitabu cha Maombolezo
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la usimamizi wa Mazingira NEMC, DK.Samuel Gwamaka akisalimiana na wadau mbalimbali pembeni yake ni Mwanasheria wa NEMC Eche Saguda akisikiliza kwa makini
Inspekta Jenerali wa Polisi Mstaafu, Omary Mahita akisaini katika kitabu cha Maombolezo Nyumbani kwa Marehemu Kinondoni
Viongozi wa Vyama Vya Siasa Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wanachi Cuf, Prof Ibrahim Lipumba na kulia kwake ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa wa CCM Keisha
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...