Na Emanuel Madafa,Mbeya
Serikali imeliataka baraza la biashara Mkoa wa Mbeya kuanza majadiliano ya pamoja kati ya sekta binafsi na serikali kuhusu masuala ya uwekezaji.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Albert Chalamila wakati akizingumza na wajumbe baraza jipya la biashara Mkoani Mbeya .
Amesema lazima kuwepo na majadiliano ambayo yatawezesha wawekezaji wa ndani na nje ili kufahamu sera na vikwazo Mbalimbali katika hatua za uwekezaji.
“Kati ya sekta binafsi na sekta za umma inapotokea tunafanya kazi kwa pamoja kwa njia ya majadiliano kunauwezekano mkubwa tukajadili changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa kikwazo kwa wawekezaji hasa masuala ya tozo na kodi “Amesema Chalamila
Ameeleza kuwa sekta binafsi inaweza kuwa na mchango kubwa kwa kuishauri serikali juu ya mazingira bora ya uwekezaji.“Serikali ikiwa imenyamaza na kutumia mabavu katika kuendesha manaake itabidi sasa watu wasiwe wawekezaji wala wafanyabiashara “Amesema Mkuu wa Mkoa .
Aidha Chalamila amelitaka baraza hilo kuandaa na kutoa taarifa kwa wawekezaji kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo katika Mkoa wa mbeya .
Kwa wake Mwenyekiti wa Chama Cha wenye viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Mkoa wa Mbeya Dkt . Lwitiko Mwakalukwa amesema baraza la biashara ni muhimu zaidi kuwepo hasa katika Maendeleo ya biashara na uwekezaji Nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya (Mwenye shati jeupe) katika picha ya pamoja na wajumbe wapya wa baraza la biashara Mkoa Mbeya
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Albert Chalamila akizungumza na wajumbe wa Baraza jipya la biashara Mkoa wa Mbeya (hawapo pichani)katika Ukumbi wa Mkapa .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...