Shirika la Viwango Tanzania (TBS), limeendelea na ukaguzi wa bidhaa sokoni kwa kushtukiza ikiwa ni moja ya majukumu yake chini ya sheria Namba 2. Ya mwaka 2009. Bi. Gladness Kaseka, Afisa Masoko Mwandamizi (TBS), alisema Ukaguzi huo unalenga kuhakikisha kuwa bidhaa zinazozalishwa na kusambazwa sokoni kwa mlaji au mtumiaji wa mwisho zinakuwa zimekidhi matakwa ya kiwango husika.
Vilevile ukaguzi huu unaenda sambamba na kuchukua sampuli ili kwenda kupima maabara ili kujihakikishia ubora wake na pia kuzitoa sokoni zile zilizozuiliwa kama nguo za ndani za mitumba na vilainishi aina ya dot 3.
Tunawahimiza wazalishaji na wasambazaji kufwata utaratibu ili kulinda soko na kuepuka hasara.
Bwn.Medard Muna Afisa Udhibiti Ubora wa (TBS) akiangalia maelezo ya msingi yanayotakiwa kuwepo katika bidhaa ya juisi na pombe kali(ujazo,tarehe ya uzalishwaji, mzalishaji ni nani,mwisho wa matumizi, jinsi ya kuhifadhi)wakati wa ukaguzi wa bidhaa sokoni wilayani Mikumi.Sampuli zilinunuliwa kwa ajili ya kupimwa ili kuhakiki ubora wake
Subira Mshery Afisa Udhibiti Ubora wa (TBS) akiangalia maelezo ya msingi yanayotakiwa kuwepo katika bidhaa ya pipi (,tarehe ya uzalishwaji, mzalishaji ni nani,mwisho wa matumizi,)wakati wa ukaguzi wa bidhaa sokoni wilayani Gairo.Sampuli zilinunuliwa kwa ajili ya kupimwa ili kuhakiki ubora wake
Venance Colman na Subira Mshery, wakaguzi wa TBS, wakiangalia maelezo ya msingi yanayotakiwa kuwepo katika taulo za watoto na za wanawake (uzito,imezalishwa lini, mzalishaji ni nani, na mwisho wa matumizi)wakati wa ukaguzi wa bidhaa sokoni wilayani Mikumi,pia sampuli ilinunuliwa kwa ajili ya kupimwa ili kuhakiki ubora wake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...