Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amesema kuanzia Jumatatu ya June 03 mwaka huu ni marufuku kwa mfanyabiashara wadogo (machinga) ndani ya mkoa huo kufanya biashara bila vitambulisho maalumu vya utambuzi vilivyotolewa na Rais Dkt. John Magufuli.
RC Makonda amesema kwa kuanzia June 3 utaanza msako wa kuwakamata wafanyabiashara wasiokuwa na vitambulisho ndani ya mkoa huo na kwakuwa walipatiwa muda wa kutosha wa kujisajili na kupatiwa vitambulisho hivyo.
Hatua hiyo imekuja baada ya Makonda kubaini uwepo wa wafanyabiashara wanaoendesha shughuli za umachinga bila kuwa na vitambulisho na hiyo ni baada ya kufanya ziara katika mitaa 9 na kubaini kuwepo kwa wafanyabiashara wengi wanaofanya shughuli zao bila vitambulisho vya utambuzi jambo ambalo sio matarajio ya serikali.
Kutokana na hilo amewataka wafanyabiashara wasiokuwa na vitambulisho kufika ofisi za wakuu wa wilaya kuanzia leo Mei 29 ili waweze kusajiliwa na kupatiwa vitambulisho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...