Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

UBALOZI wa Uswisi nchini Tanzania umetoa zaidi ya milioni 170 kwa ajili ya kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa kuhifadhi mazingira kupitia sanaa.

Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam, Balozi wa Uswisi nchini Florence Mattli amesema kuwa fedha hizo ni jitihada za kuchangia ukuaji wa sekta ya sanaa na utamaduni nchini Tanzania kwa mashirika na vikundi kupata fedha hizo na kuonesha vipaji vyao.

Amesema, Shirika la maendeleo na Ushirikiano la Uswisi kupitia programu yake ya utamaduni ilitoa wito wa mapendekezo ulioitwa Taka Yangu hazina yangu unaolenga kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira.

"Taka yangu, Hazina yangu inatoa wito kwa kila mtu kuangalia taka kwa mtazamo tofauti, kwani taka zingine zinaweza kuwa na thamani iwapo zikitumika tena kwa njia nyingine," amesema Florence.

"Lengo la mradi huu ni kutafakari kwa kutumia sanaa juu ya tabia zetu na wajibu wetu kama raia, namna tunavyotumia na kutupa taka inaweza kuwa na athari za mazingira yetu,"

Mkurugenzi wa Makumbusho Achiles Bufure amesema kuwa mradi huu utasaidia katika kutunza na kuboresha mazingira na takataka na kuwa fursa.Bufure amesema, kwa kipindi cha miaka mitatu Ubalozi wa Uswisi wamekuwa wanashiriki kwenye masuala ya Kijamii ambapo walianza na Masuala ya rushwa, mimba za utotoni na sasa hivi mazingira.

Mbali na hilo, amesema watashirikiana na wasanii kutumia sanaa kuleta maendeleo na mradi wao unaangalia zaidi kuwa takataka ni dili na fursa kwa maendeleo ya nchini.Kwa upande wa Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Adrian Nyangamale amesema wasanii wanapopewa fedha hizo wanatakiwa wakafanyie kazi kwa ajili ya maendeleo na kutumia sanaa walizonazo kama fursa ya ajira.

" mradi huu unalenga kuboresha taka kuwa fursa kupitia sanaa kwani takataka zimekuwa kikwazo kikubwa tofauti na nchi zingine," amesema Nyangamale.Aidha, ametoa pongezi kwa Ubalozi wa Uswisi katika ushiriki wao wa masuala ya kimaendeleo na kuonesha ni namna gani wanapambana kuhakikisha tunatoka hapa tulipo na kwenda mbele zaidi kiuchumi na kimaendeleo.

Naye Kiongozi wa Kikundi cha Wasanii 14+, Twahiri Sabuni amewashukuru ubalozi wa Uswisi kwa kupata nafasi hiyo na kuwa moja ya vikundi vitano vilivyopata nafasi ya kuonesha ubunifu wao kupitia takataka na kutengeneza kazi za sanaa kubwa matumizi mbadala.

Amesema, watashirikiana na wanamchi, watoto, vijana na watu wenys uhitaji maalumu katika kutimiza azma ya kulinda mazingira na kutumia taka kama fursa ga kiuchumi.Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania umekuwa ukichangia katika kuendeleza masuala mbalimbali ya utamaduni wa Tanzania tangu mwaka 2005 na kutoa asilimia 1 ya bajeti yake kuunga mkono sekta ya sanaa na utamaduni.

Mashirika na vikundi vilivyofanikiwa kupata fedha hizo baada ya kupelekea maombi ni pamoja na Makumbusho ga Taifa la Tanzania, CDEA, Chuma Art Worksho, Alama Art and Media Production na Wasanii 14+ na aina mbalimbali za sanaa zitatumika katika uhamasishaji na kufikia kwenye mikoa mballimbali nchini.
 Balozi wa Uswisi Nchini Tanzania Florence Mattli akikabidhiana mkataba na  Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa Achiles Bufure  kwa ajili ya kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa kuhifadhi mazingira kupitia sanaa. Ubalozi huo umetoa kiasi cha Shillingi Milioni 170 kwa mashirika na vikundi vitano nchini vitakavyotumia takataka na kuzigeuza fursa wakitumia kauli ya  Taka Yangu hazina yangu unaolenga kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira.

 Balozi wa Uswisi Nchini Tanzania Florence Mattli akipeana mkono na  Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa Achiles Bufure, Kulia ni Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Adrian Nyangamale baada ya makabidhiano ya mkataba   kwa ajili ya kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa kuhifadhi mazingira kupitia sanaa. Ubalozi huo umetoa kiasi cha Shillingi Milioni 170 kwa mashirika na vikundi vitano nchini vitakavyotumia takataka na kuzigeuza fursa wakitumia kauli ya  Taka Yangu hazina yangu unaolenga kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira.
Balozi wa Uswisi Nchini Tanzania Florence Mattli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mashirika na vikundi vilivyofanikiwa kuingia kwenye mradi wa  umuhimu wa kuhifadhi mazingira kupitia sanaa. Ubalozi huo umetoa kiasi cha Shillingi Milioni 170 kwa mashirika na vikundi vitano nchini vitakavyotumia takataka na kuzigeuza fursa wakitumia kauli ya  Taka Yangu hazina yangu unaolenga kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...