Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha
Wajasiriamali wadogo wameiomba serikali kuwatafutia Muwekezaji atakaewaletea mashine za kutengeneza vifungashio pamoja na lebo ili kupunguza usumbufu na adha wanayoipata.
Iwapo tutapata vifungashio bora na vizuri itasaidia kukuza biashara yetu na kufanya bidhaa zetu kuwa kuwa zenye ubora Kitaifa na Kimataifa zaidi.
Hayo yamebainishwa leo na Mjasiliamali Annet Kivuyo alipokuwa akizungumza katika semina ya wajasiliamali ilioandaliwa na shirika la Uthibiti wa Viwango (TBS) kwa kushirikiana na SIDO, ambapo alisema kuwa changamoto ya vifungashio inachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza soko la bidhaa za hapa nchini kwa sababu vifungashio vyetu havipo kwenye ubora unao kubalika.
"vifungashio bora vya kuvutia vitasaidia bidhaa zetu ziwe kwenye viwango vyenye ubora , serikali itusaidie tuwe na mtu atakae wekeza mashine za lebo na kutengeneza vifungashio kama wenzetu wa nchi jirani, kwani kwa sasa tunaagiza nchi za nje na vinavyokuja pia vinakuwa vichache havitoshelezi mahitaji ni gharama kubwa inatumika"alisema Annet
Alisema Tanzania inabidhaa nzuri na zenye ubora, ila changamoto kubwa inayotusumbua ni vifungashio, hivyo ameiomba Serikali ijitahidi kupata mwekezaji atakae saidia kuondoa tatizo hilo.
Kwa upande wake Mmkurugenzi wa TBS Jabir Abdi alisema kuwa wameamua kufanya mafunzo hayo kwa wafanyabiashara wachakataji wa bidhaa za ngozi, lakini pia huo ni muendelezo wa kuhakikisha wanapata elimu sahihi itakayo wasaidia kufikia viwango vya Kitaifa ili waweze kuuza bidhaa zao, sio tu hapa nchini pia waweze kuuza nje ya nchi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...