Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ( kulia), akisalimiana na Meneja wa
Benki ya Biashara ya DCB Tawi la Dodoma, joseph Njile wakati
Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Godfrey Ndalahwa (katikati),
akimtembelea waziri mkuu, ofisini kwake, bungeni Dodoma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ( kulia), akimsikiliza Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (katikati)
pamoja na baadhi ya maofisa wa benki hiyo, walipomtegembelea waziri
mkuu, ofisini kwake, bungeni Dodoma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ( katikati), akipiga picha na Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (wa pili
kushoto) pamoja na baadhi ya maofisa wa benki hiyo, walipomtembelea
waziri mkuu, ofisini kwake, bungeni Dodoma jana. Kutoka kushoto ni,
Rahma Ngassa, Joseph Njile na Nuru Ashraf (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu).
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameupongeza uongozi benki ya DCB kwa
kufanikiwa kubadili muundo kutoka benki ya jamii na kuwa ya biashara
kwani kuna benki nyingi ambazo zimeshindwa kujiendesha.
Akizungumza na uongozi wa benki hiyo, alipokutana na uongozi wa benki
hiyo ofisini kwake Bungeni jijini Dodoma, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
amesema benki nyingi za jamii zimekufa baada ya kushidwa kujiendesha
lakini kwa benki ya DCB wameweza kumudu kujiendesha hadi kufikia kuwa
benki ya biashara.
Hata hivyo, Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa benki hiyo uimarishe
kitengo cha elimu kwa umma ili jamii ifahamu huduma
wanazozitoa."Nendeni kwa wananchi mkawape elimu kuhusu umuhimu wa
kufungua akaunti na pia rahisisheni mazingira ya kutolea huduma kwa
wateja."
Pia Waziri Mkuu ameitaka benki hiyo isogeze huduma kwa wananchi
hususan maeneo ya pembezoni ambayo bado hayajafikiwa. Amesema ni
muhimu wananchi wakasogezewa huduma za kibenki ili waweze
kuhakikishiwa usalama wao pamoja na fedha zao.
Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Godfrey Ndalahwa amesema
tangu benki hiyo ianzishwe imefanikiwa kukuza amana za wateja kutoka
Sh. bilioni mbili mwaka 2002 hadi Sh. bilioni 75 Desemba mwaka 2018. Pia
mikopo imeongezeka kutoka Sh. bilioni moja mwaka 2002 na kufikia Sh.
bilioni 90, Desemba 2018, faida ikiwa ni Sh. bilioni 17.7 baada ya kodi.”
Mkurugenzi huyo alisema katika kipindi cha miaka 16 ya utendaji wake,
benki hiyo imeshatoa gawio la zaidi ya Sh. bilioni 11 kwa wanachama wake
huku akitumia nafasi hiyo kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano
inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli kwa kuboresha maendeleo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...