Benki ya Exim leo imewatangaza washindi wake watano watakaoungana na watanzania wengine kwenda kuishangilia timu ya taifa ‘Taifa Stars’ katika mashindano ya fainali za Kombe la Mataifa ya Africa (Afcon) 2019 nchini Misri.
Kampeni hiyo maalum inayofahamika kama “Deposit & Win – Twende Tukaliamshe Misri” ilikuwa inatoa fursa kwa wateja wa benki hiyo kulipiwa gharama zote za safari na malazi ili waweze kushuhudia mechi za timu ya taifa, Taifa Stars katika mashindano hayo.
Washindi hao wa Kampeni ya “Deposit & Win – Twende Tukaliamshe Misri” watapata fursa ya kulipiwa gharama zote za safari ya kwenda na kurudi Misri, malazi na gharama za kujikimu na ili kuweza kushuhudia mechi za timu ya taifa, Taifa Stars katika mashindano hayo.
Washindi waliotangazwa leo hii ni Bw Musa Mohamed (Mtwara) Bw Athumani Hassani (Manyara), Bw Deogratius Kessy (Arusha), Bi Msimu Ngaruka (Dar es Salaam) pamoja na Bw Justine Tembo (Arusha) ambao wamepatikana kupitia droo kubwa ya kampeni hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam mapema hii leo chini ya uangalizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT)
Akizungumza baada ya kupatikana kwa washindi hao Mkuu wa huduma ya rejareja wa benki ya Exim, Bw. Andrew Lyimo alisema washindi hao watapata fursa ya kuungana na Taifa Stars katika mashindano Afcon nchini Misri huku wakiwa wamelipiwa gharama zote za safari ikiwemo gharama na Visa, tiketi ya ndege, gharama za tiketi ya kushuhudia mechi hizo pamoja na fedha za kujikimu.
Kwa mujibu wa Bw. Lyimo ili kushiriki katika kampeni hiyo, wateja wapya walipaswa kufungua Akaunti ya Akiba na kuhakikisha kila mwezi ina kiasi kisichopungua Tshs 500,000 au zaidi au kufungua Akaunti ya Current/biashara ikiwa na wastani wa kila mwezi wa Tshs 10,000,000 au hifadhi ya amana maalum (Fixed deposit) yenye thamani isiyopungua Tshs 5,000,000.
“Kwa wateja ambao tayari wana akaunti ya benki ya Exim walichotakiwa kufanya ni kuongeza akiba kwa kiasi cha Tshs 500,000 au zaidi kwa Akaunti za Akiba au kuongeza kiasi cha Tshs 10,000,000 kwenye akaunti zao za Current/biashara au kuwa na hifadhi ya amana maalum (Fixed deposit) yenye thamani isiyopungua Tshs 5,000,000.’’ alibainisha
Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim, Stanley Kafu, alisema kampeni hiyo inatoa nafasi kwa washindi hao kuweza kushuhudia Taifa Stars ikitimiza ndoto zake za kushiriki katika mashindano ya AFCON baada ya zaidi ya miaka 39 kupita.
Kwa mujibu wa Bw Kafu, kampeni hiyo ni sehemu ya mkakati wa kibenki katika kutafuta kesho bora kwa wateja wake na jamii kwa ujumla ambapo pamoja na mambo mengine benki hiyo imekuwa ikiunga mkono agenda za kitaifa ikiwemo suala zima la michezo.
Meneja
Masoko na Mahusiano ya jamii wa Benki ya Exim, Bw Abdulrahman Nkondo (Katikati) akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani) wakati
akitangaza washindi Kampeni maalum ya benki hiyo inayofahamika kama “Deposit
& Win – Twende Tukaliamshe Misri” watakaoungana na watanzania wengine
kwenda kuishangilia timu ya taifa ‘Taifa Stars’ katika mashindano ya fainali za
Kombe la Mataifa ya Africa (Afcon) 2019 nchini Misri. Wengine ni pamoja Msimamizi Mkuu wa Matawi wateja wa
rejareja wa benki hiyo Bw Mwinyimkuu Ngaliama (Kulia) pamoja na Mkaguzi kutoka
Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT) Bw Abdallah Hemedy
Msimamizi
Mkuu wa Matawi, Kitengo cha wateja wadogo na wakati (Cluster Head) wa benki ya
Exim Tanzania Bw Mwinyimkuu Ngaliama
(Kulia) akizungumza
wakati wa droo hiyo.
Msimamizi
Mkuu wa Matawi, Kitengo cha wateja wadogo na wakati (Cluster Head) wa benki ya
Exim Tanzania Bi. Gertrude Mbunda (kulia) akizungumza kwenye droo hiyo.
Timu
ya maofisa kutoka benki ya Exim Tanzania pamoja na msimazi kutoka Bodi ya
Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT) Bw. Abdallah Hemedy wakiendesha kwa
umakini droo hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...