NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
BODI ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), pamoja na Menejimenti ya Mamlaka hiyo, zimemefanya ziara kwenye kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere ili kujionea jengo jipya la kiwanja hicho, Terminal III (TBIII), pamoja na Maktaba mpya na ya kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani.
Ziara hiyo iliyofanyika Ijumaa Juni 21, 2019 pia iliwahusisha wajumbe wa Kamati ya Maudhui ya TCRA.
Akizungumzia nia ya ziara hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James M. Kilaba alisema, Mamlaka kama Mdhibiti na Msimamizi wa Mawasiliano nchini, imeona ni vema kutembelea taasisi hizo mbili kwani kuna mambo ya msingi yanayofanywa na taassi hizo yanahusiana moja kwa moja na huduma zinazotolewa na TCRA.
“Lengo la ujio wetu hapa Terminal III nikuangalia katika hatua hizi ambazo ujenzi umekamilika ni mahitaji yapi ambayo bado ili sisi tuongeze ushiriki wetu ili kuyakamilisha hususan katika mifumo ya mawasiliano.” Alsiema Mhandisi Kilaba.
Alisema wakiwa hapo TBIII wamepata fursa ya kuulizia hali ya mawasiliano kama imekamilika ambapo watoa huduma, TTCL, Airtel, Vodacom, Tigo, Zantel, Halotel na hata Internet kama wako tayari.
“Huduma hizi ni muhimu sana na zinatakiwa ziwe kwenye maeneo kama haya kwa sababu zinawezesha hata kufanya utalii kuwa rahisi, mgei anapoingia hapa na anataka kwenda eneo Fulani la utalii lazima awasiliane, lakini pia TCRA inatoa masafa kwa ajili ya kuongozea ndege zinapotua na kuruka na lengo hasa ni kuhakikisha hakuna muingiliano katika huduma hizo." Alibainisha Mkurugenzi huyo Mkuu wa TCRA.
"Kuja kwetu kumetupa fursa ya kujifunza mengi kama ambavyo watanzania wanaweza kushuhudia kuwa kiwanja hiki ni kizuri, kinapendeza na mawasiliano yapo yanaendelea kukamilishwa na tumejionea hata Wifi point ipo.” Alifafanua Mhandisi Kilaba.
Aidha kuhusu Maktaba mya ya kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mhandisi Kilaba alisema, Maktaba hiyo inatumia huduma za TCRA kwani moja ya huduma zitolewazo ni pamoja na Maktaba mtandao (e-library) na hili ni jambo jema.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya TCRA, Dkt.Jones Killimbe alisema, ziara hiyo imekuwa ni ya mafanikio makubwa kwani imewezesha timu nzima ya TCRA, Wajumbe wa Bodi, Menejimenti, Wajumbe wa Kamati zinazosaidia kutekeleza majukumu kwenye mamlaka kwa pamoja wameelimika sana.
“Kiwanja hiki katika lugha ambayo ningeiazima ni flagship project….ni mradi wa kimkakati wa taifa hili... nikisema kimkakati ni kwasababu mojawapo ya masuala ya kiuchumi ya nchi yetu ni utalii, na nadhani huu utakuwa mlango mkubwa sio dirisha…utakuwa mlango mkubwa wa utalii na mchango wa utalii kwenye uchumi wetu utaongezeka sana.” Alisema Dkt. Killimbe.
Ziara hiyo imewezesha wajumbe kupata maelezo ya kina ya kukamilika kwa huduma mbalimbali kwenye jengo la TBIII hali kadhalika kwenye maktaba ya ksiasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaa,
Mwenyekiti
wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jones Killimbe
(mwenye shati jeupe), Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Mhandisi James M.
Kilaba, (kulia), wajumbe wa Bodi na Kamati ya Maudhui ya TCRA
wakiongozwa na Msimamizi wa Mradi wa ujenzi wa jingo la Terminal 3
(TBIII) la kiwanja cha ndege cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
Juni 21, 2019.
Dkt.
Jones Killimbe (kushoto) na Mhandisi Kilaba, wakitembelea eneo la
kusubiri abiria la jingo la TBIII kabla ya kuingia ndani ya ndege.
Muonekano
wa nje wa eneo la kuondokea abiria kwenye jingo jipya la TBIII la
kiwanja cha ndege cha Julkius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Ujumbe
wa TCRA ukipatiwa maelezo na Mhandisi Barton Komba (kulia), kuhusu wapi
abiria anapaswa kuelekea mara tu baada ya kuingia eneo la kuondokea
abiria.
Mandhari ya sehemu ambayo abiria wa kawaida watakuwa wakisubiri kabla ya kupanda ndege.
Eneo la udhibiti wa Pasipoti mara tu baada ya abiria kuwasili kwenye kiwanja hicho.
Mhandisi Komba (kushoto), akimpitisha Mkurugenzi Mkuu wa TCRA eneo litakalotumika kudhibiti pasipoti.
Mjumbe
wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Bw. Jacob Tesha, akizunhumza jambo ili
kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya huduma kwenye jingo hilo.
Eneo la ku chek-inn.
Picha ya pamoja.
Msimamizi
wa Maktaba mpya na ya kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (eneo la
nyaraka za serikali), akitoa maelezo kwa ujumbe wa TCRA ukiongozwa na
Mwenyekiti wa bodi, Dkt. Jones Killimbe (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka hiyo, Mhandisi James M. Kilaba (mwenye nguo za kibuluu), wakati
wa ziara ya kutembelea maktaba hiyo.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Maudhui, TCRA), Bi. Valerie Msoka (kushoto) na mmoja wa
wajumbe wa Kamati hiyo, Bw. Dreck Murusuri, wakiangalia jinsi maktaba ya
kielektroniki (e-library)ya Maktaba ya kisasa ya UDSM inavyofanya kazi.
Mkurugenzi Mkuu, TCRA, Mhandisi James M. Killaba (wapili kulia), akiangalia kwa makini jinsi maktaba ya kielektroniki (e-library) ya Maktaba ya kisasa ya UDSM inavyofanya kazi.
Mwenyekiti
wa bodi, Dkt. Jones Killimbe (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
hiyo, Mhandisi James M. Kilaba (mwenye nguo za kibuluu), pamoja na
ujumbe wakiouongoza, wakiwa kwenye chumba cha maktaba ya kielektroniki
(e-library) ya Maktaba hiyo ya kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Maktaba mpya ya kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),
Dkt.Esther Ndenje Sichalwe (katikati), akiongoza ujumbe wa TCRA
ulipotembelea maktaba hiyo Juni 21, 2019.
Dkt.
Sichalwe (kulia), akizungumza na Kaimu Mkuu wa Kitenmgo cha Mawasilian,
Uhusiano na Elimu kwa Umma, TCRA, Bw. Semu Mewakyanjala, wakati wa
ziara hiyo.
Picha ya pamoja ya ujumbe wa TCRA mara baada ya kutembelea maktaba hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...