Na Dennis Buyekwa

Mahakama ya Afrika ya Mashariki imetupilia mbali maombi ya dharura katika Shauri namba 2 la mwaka 2019 lililofunguliwa na Viongozi waandamizi wa vyama vya siasa vya upinzani nchini katika Mahakama hiyo iliyopo jijini Arusha.

 Mahakama imechukua uamuzi huo baada ya upande wa walalamikaji kumuomba Jaji anayesikiliza kesi hiyo Mhe. Monica Mungenyi kusikiliza upande mmoja wa walalamikaji kitendo kilichopingwa na mawakili wa Serikali.


Baada ya kusikiliza shauri hilo kwa kuzingatia ushahidi uliotolewa na upande wa waleta maombi, Jopo la waheshimiwa Majaji liliamua kutupilia mbali shauri hilo kwa kile walichokieleza kuwa upande wa waleta maombi wameshindwa kuthibitisha kwa Mahakama hiyo umuhimu wa kusikiliza shauri upande mmoja kwani masuala yaliyopo katika shauri hilo ni muhimu hivyo ili haki itendeke ni vyema upande wa pili usikilizwe ndipo Mahakama itoe maamuzi.

Kesi hiyo iliyosikilizwa na Majaji watano wa Mahakama hiyo ambao ni Mhe. Jaji Monica Mugenyi, Mhe Jaji Faustine Ntezyilyayo, Mhe Jaji Fakihi Jundu, Mhe. Jaji Audace Ngiye, na Mhe. Jaji Charles Nyachae, ilifunguliwa na viongozi wa vyama vya siasa wakiongozwa na Mhe. Freeman Mbowe, Mhe. Zitto Zuberi Kabwe, Mhe.Hashimu Rungwe, Mhe.Seif Sharif Hamad na Mhe.Salum Mwalim kupinga utekelezaji wa sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 2019.

Kufuatia hatua hiyo waheshimiwa Majaji wameutaka upande wa waleta maombi kuipatia nakala ya maombi hayo Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ili kujibu, na tarehe ya kusikiliza maombi hayo itapangwa hapo baadae.

Katika shauri hilo upande wa Serikali uliwakilishwa na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kupitia Mawakili wa Serikali Ndg. Evarist M. Mashiba, na Bw. Kombe wakati upande wa Mashtaka uliwakilishwa na Bi. Fatma Karume, Bw. Jebra Kambole na Ndg, John Malya.
Wakili Mkuu wa Serikali


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...