Muoenekano wa baadhi ya majengo yanayoendelea kujengwa katika kituo cha Afya Mkonze Jijini Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Mb) akikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Afya Mkonze kilichopo Jijini Dodoma.
……………………

Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amekasirishwa na kasi isiyoridhisha ya ujenzi wa kituo cha Afya Mkonze Jijini Dodoma ambachokwa mujibu wa ratiba za ujenzi kinatakiwa kukamilika Juni 30, 2019.

Waziri Jafo ameonyesha hali hiyo wakati alipotembelea KItuo cha Afya Mkonze kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kimepokea fehda za ujenzi Tsh Mil 400 mapema mwezi Disemba, 2018
“Sikutegemea kukuta kituo cha Mkonze kikiwa katika hali hii, kituo hiki ni miongoni mwa vituo vilivyopelekewa fedha mapema tu na kiko mjini tena Makao Makuu ya Nchi mnashindwa na Halmashauri ambazo ziko pembezoni huko na zina chanagmto nyingi lakini wameshakamilisha ujenzi nini kinakwamisha ujenzi wa kituo hiki

Kituo hiki cha Mkonze kilitakiwa kiwe cha mfano, ujenzi ukamilike mapema kwa sababu kila kitu kiko karibu yenu, vifaa vya ujenzi mnavipata kwa urahisi, hakuna changamoto ya usafiri ili mfike hapa hata Ofisi ya TAMISEMI iko hapa hapa sasa endapo mmekwama kitu mna njia nyingi za kutatua nashidnwa kuelewa kwanini mpaka leo bado mnasua sua kukamilisha ujenzi wa kituo hiki” alisema Mhe. Jafo.

Waziri Jafo aliongeza kuwa Wananchi wanataka huduma za Afya hawataki hadithi Mnatakiwa kuongeza kasi ya ujenzi na kukamilisha majengo yote yanayotakiwa tena kwa ubora wa hali ya juu na ifikapo Juni, 30 kituo hiki kikwe kimeshakamilika.

Naye Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi amesema kuwa fedha walizopokea ni Tsh Mil 400 kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho lakini kutokana na hadhi ya Jiji waliona watafute fedha zaidi ili kufanya Kituo hicho kiwe na ubora sawa na vituo vingine vilivyojengwa Jijini Dodoma.

“Tumeongeza Tsh Mil 100 kutoka katika mapato ya ndani ya Halmashauri sasa fedha hizi zilichelewa kufanyiwa mabadiliko kwenye bajeti “Realocation” hiyo ndiyo sababu pekee iliyopelekea kuchelewa kwa baadhi ya kazi za ujenzi katika kituo hiki cha Mkonze; Lakini kwa sasa tumeshafanikiwa kuhamisha izo fedha na tumepokea maelekezo na tutasimamia kuhakikisha kituo hiki kinakamilika ndani ya muda uliopangwa” Alisema Kunambi.

Ofisi ya Rais Tamisemi inatekeleza Mpango wa Maboresho wa Huduma za Afya ambapo Vituo vya kutolea huduma za Afya 352 vipo katika hatua mbalimbali zaukarabati, ujenzi na ukamilishaji. Kazi hii imefanyika kwa awamu tano.

Kati ya hivyo 304 ni Vituo vya Afya ambavyo vitatoa huduma za dharura ya upasuaji kwa mama mjamzito.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...