Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha
KAMPUNI ya Candy & Candy imetoa misaada wa vyakula, vinywaji baridi
na fedha za kununulia nguo za ndani watoto yatima wanaolelewa kwenye
kituo cha Faraja cha jijini Arusha.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Joe Kariuki aliongoza wafanyakazi wa kampuni
hiyo kugawa vitu hivyo pamoja na kuongea na watoto wa kituo hicho zaidi ya 200.
Alisema kuwa kampuni ya Candy & Candy itaendelea kuwa karibu na kituo
hicho ambapo aliahidi kurudi kituoni hapo baada ya miezi miwili na
endapo akiwakuta wamebadilika na kuwa na mwenendo mwema basi
atawapatia zawadi ya luninga.
"Baba yenu (Faraja) ameniambia hapa kuna waliokuwa wamehukumiwa na
kufungwa, tunashukuru sasa mko kwenye hiki kituo mnalelewa vizuri basi
badilikeni tabia ili msirudi tena kule kwenye matatizo," alisema
Kariuki na kuongeza.
"Nitakuja hapa baada ya miezi miwili, baba yenu akiniambia
mmebadilika tabia, hampigi watoto wa majirani na mnafanya usafi wa
mwili (kuoga) nitawanunulia TV nitaifunga hapo (akionyesha
ukutani),".
Walikabidhi kituoni hapo kilo 100 za mchele, unga wa mahindi gunia nne, mafuta ya kupikia ndoo mbili zenye lita 20 pamoja na juisi na biskuti ambazo waliwagawia watoto kituoni hapo.
Mkurugenzi huyo wa Candy& Candy ambaye kampuni hiyo ina matawi nchi
mbalimbali huku makao makuu yake yakiwa nchini Uingereza alitoa fedha
kwa ajili ya kusaidia masomo ya ziada ya mwanafunzi, Baraka Eli ambaye
alidai kuwa endapo asingelipa kwa siku ya Jumatatu basi asingeruhusiwa
kuingia darasani kujifunza.
Kariuki alilazimika kutoa fedha kwa ajili ya kuwanunulia nguo za ndani watoto
wenye umri wa kati ya miaka tisa na 16 kwenye kituo hicho baada ya
kumweleza kuwa wengi wanayo moja huku wachache wakiwa na ambazo
hazizidi tano.
Naye Rais wa programu ya U & I, (you and I) inayoendeshwa na Candy &
Candy, Nasra Swai akiongea na watoto wenye umri wa kati ya miaka tisa
na 17 aliwaleza umuhimu wa kujitambua kama watoto.
Aidha ali waeleza watoto hao jamii inawapenda na kuwathamini ndiyo
sababu wamefika kwenye kituo hicho kuongea nao na kubadilishana
mawazo ambapo aliwaahidi kurudi tena kwenye kituo hicho kwa ajili ya
kuzungumza nao juu ya masuala mbalimbali ya makuzi.
Akiongea kwa niaba ya watoto kwa niaba ya wenzake mtoto, Barakaeli
Faraja alisema kuwa wanashukuru kampuni hiyo kuwasaidia kupata vitu
hivyo kwani wmekuwa wakivihitaji kwa muda mrefu.
Aliiomba kampuni hiyo iangalie uwezekano kuwasaidia zaidi kuwalipia
ada baadhi ya watoto, kupata vitanda kwani kwa sasa wanabanana mno,
kompyuta na runinga kwa ajili ya chumba cha watoto wakubwa.
Mkurugenzi wa kituo hicho, Faraja Mollel alisema kuwa wanakabiliwa na
changamoto kubwa ya ukosefu wa chakula cha kutosha kwa ajili ya watoto
hao ambapo wakati mwingine huwapa milo miwili tu kwa siku.
Alisema kuwa yeye aliguswa kuanzisha kituo hicho kutokana na historia
ya maisha yake ambapo yeye akiwa na umri mdogo aliwahi kuishi kwenye
mitaa ya jiji la Arusha akiwa na dd yake, Jenipher ambaye kwa sasa
anaishi Marekani.
Alisema kuwa walipata msamaria mwema mama wa Kizungu ambaye
aliwachukua na kwenda kuishi nao ndipo maisha yao yalipobadilika hivyo
baada ya kufanikiwa akaguswa kuwasaidia watoto waliopitia magumu kama
ya kwake.
Faraja alisema kuwa awali kwnye kituo hicho hapakuwa na shida ya ada
kwa watoto a kituo hicho kwani kulikuwa na mfadhili ambaye alikuwa
akiwasaidia kununua chakula na kulipia ada baadhi ya watoto hao lakini
alifariki mwaka jana jambo linalowaweka katika wakati mgumu kwa sasa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...