Wakazi wa Dodoma na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi katika kampeni  ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni  na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa ajili  ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.

Mkuu wa TCRA Kanda ya Kati  Mhandisi Antonio  Manyanda amesema ni fursa kwa wananchi wa Dodoma kupata huduma kutokana na kuwa na mnyororo wadau wa  mawasiliano. 

Amesema kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano. 

Manyanda amesema kuwa wananchi wasio kuwa na Vitambulisho vya NIDA wahakikishe  wanapata katika usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole. 

"TCRA iko karibu na wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo"amesema Manyanda.
 Wananchi wakikamilisha usajili wa Laini za Simu kwa Kutumia alama za vidole. Katika Mnada jijini Dodoma.

 Wananchi wakiwa katika Mnada na kupata huduma za mawasiliano katika Mnada huo jijini Dodoma.
 Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Bidhaa za Mawasiliano  Thadayo Ringo akitoa  maelekezo kwa Wananchi wa Dodoma  katika  kampeni ya Mnada kwa Mnada inayoendeshwa na TCRA
 Mwananchi wa Dodoma  akiweka alama za vidole kwa ajili ya laini za simu.
Timu ya TCRA  ikiwa katika picha ya pamoja  katika kampeni  ya Mnada kwa Mnada  jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...