Kaimu Meneja wa Bandari ya Mwanza,Geoffrey Lwesya akizungumza na waandishi wa habari leo Wilaya ya Sengerema Halmashauri ya Buchosa jijini Mwanza, ambapo mamlaka ya bandari Tanzania(TPA) inajenga gati ya kisasa katika Mwalo huo kupunguza adha ya Wanawake Watoto na Wazee kupanda kwa shida katika boti zinazo fanya safari kutokea hapo kwenda visiwani. Waandishi wa Habari wapo katika ziara ya kutembelea na kutangaza miradi ya maendeleo ya bandari zilizo katika Ziwa Victoria, Tanganyika na Nyasan na kujionea maboresho yaliyo fanywa na TPA Katika awamu hii ya tano chini ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Mhandisi Abraham Msina akizungumza na Waandishi wa habari  kuhusu ya Maboresho yaliyofanyika katika Bandari ya Lushamba Wilayani Sengerema ambapo Mamlaka ya Bandari imekamilisha ujenzi wa gati ya kuegeshea Boti na Meli zinazofanya safari katika ziwa victoria kutoka eneo hilo kwenda visiwa vya ukara na vinginevyo.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Lushamba Wilaya Sengerema akishukuru Serikali ya Awamu ya tano chini ya Dk. John Pombe Magufuli kwa kuwaondolea kero ya usafiri kwa kujenga gati ya kisasa na sehemu za kupumzikia abiria na jengo la mizigo katika Bandari ya Lushamba

Mmoja wa Wakazi wa Buchosa Wilaya ya Sengerema akipanda boti kwa shida,kama alivyonaswa na mpiga picha wa Globu ya Jamii mapema leo,akitumia ngazi kutokana na kutokuwepo kwa gati ya kupaki boti hizo ambazo zimekuwa zikisaidia suala la usafiri ndani ya ziwa victoria,hata hivyo Serikali kupitia Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), imejenga gati ya kisasa katika eneo hilo ili kuondoa adha hiyo inayowakumba wakazi wa maeneo hayo.

Sehemu ya gati ya kupaki boti hizo ya kisasa inayojengwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania itakayoondoa adha ya usafiri kwa wakazi wa Buchosa ikiwa katika hatua za mwisho kukamilika kama inavyoonekana
Jengo la kuhifadhia Mizigo katika Bandari ya Lushamba kama linavyoonekana kwa nje ambapo kwa sasa limekamilika kwa zaidi ya asilimia 90.
Jengo la kupumzikia abiria katika bandari ya lushamba ambalo limekamilika kwa zaidi ya asilimia 90 kama linavyooenekana, Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) Imefanya maboresho katika bandari ya lushamba ili kuondoa kero walizokuwa wanapata wananchi walikouwa wakitumia Mwalo huo.

Sehemu ya geti ya Bandari ya Lushamba inavyoonekana kwa nje 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...