Banda la Shirika la Reli Tanzania - TRC lilipo katika maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa umma Barani Afrika katika viwanja vya KICC jijini Nairobi nchini Kenya Limepata fursa ya kutembelewa na Waziri wa Utumishi wa Umma,Vijana na Jinsia Mheshimiwa, Dokta Margaret Kobia juni 22, 2019.
Lengo la ziara ya Waziri katika maadhimisho haya kwa nchi za bara la Afrika ni kufahamu majukumu ya taasisi za utumishi wa umma zilizoshiriki,maendeleo na ubunifu unaoleta tija katika nchi zilizoshiriki kutoka nchi tofauti barani Afrika.
Kupitia ziara hiyo Mheshimiwa Waziri alisifu uthubutu alioufanya Mh.Rais Dokta John Pombe Magufuli katika mradi wa ujenzi wa Reli ya kisasa-SGR.
Pia Waziri amepata fursa ya kufahamu Huduma zitolewazo na TRC pamoja na miradi mikubwa inayosimamiwa na Shirika la Reli yaani Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa-SGR,Uboreshaji wa Reli ya kati na miradi mingine kama Ufufuaji wa njia ya reli Tanga, Arusha ba Moshi pamoja na Mradi wa treni za kisada za Mijini ambazo TRC imeanza na jiji la Daresalaam na Dodoma.
Maadhimisho haya ya Utumishi wa umma barani Afrika yaliyobebwa na kauli mbiu Uhusiano kati ya uwezesha vijana na usimamizi masuala ya uhamiaji, kujenga utamaduni wa utawala Bora, matumizi ya Tehama na ubunifu katika utoaji utoaji huduma jumuishi.
Washiriki kutoka Tanzania ni taasisi zilizo chini ya serikali kuu ambapo maadhimisho haya yameandaliwa na kuongozwa na Ofisi ya Rais Utumishi, Taasisi hizo ni zilizoshiriki ni Shirika la reli Tanzania-TRC, Mamlaka ya chakula na Dawa-TFDA, Bohari ya Dawa Tanzania-MSD.
Maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma barani Afrika yanatarajia kufungwa juni 23, 2019 katika jiji la Nairobi nchini Kenya.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano TRC Bi Jamila Mbarouk akitoa Maelezo na ufafanuzi kwa Waziri wa Wizara ya Utumishi wa Umma, Vijana na Jinsia, Jamhuri ya Kenya Dkt.Margaret Kobia (Wa pili kushoto)kuhusu Huduma zitolewazo na TRC pamoja na miradi inayosimamiwa katika maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma mjini Nairobi nchini Kenya katika viwanja vya KICC leo juni 22, 2019.
Mhandisi Tito Mateshi kutoka TRC akitoa Maelezo kwa Bi Hytham Amour kuhusu miradi inayosimamiwa na TRC pamoja na huduma zitolewazo katika maadhimisho ya Wiki ya wiki ya utumishi wa umma jijini Nairobi nchini katika viwanja vya KICC juni 22, 2019.
Watumishi wa Shirika la Reli Tanzania -TRC wakimpokea mdau Bi Lilian John, tayari kwa kumpatia maelezo kuhusu Huduma zitolewazo pamoja na miradi inayosimamiwa na TRC katika maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma barani Afrika yanayoendelea jijini Nairobi, nchini Kenya juni 22, 2019.
Baadhi ya Wadau jijini Nairobi walipotembelea banda la Shirika la Reli Tanzania -TRC kwa ajili ya kupata uelewa kuhusu Huduma na Miradi inayosimamiwa na TRC katika viwanja vya KICC jijini Nairobi nchini Kenya juni 22, 2019.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...