Azma ya Serikali ya Awamu ya Tano kuimarisha Viwanda imeonekana kutekelezwa kwa vitendo katika vyuo vya Elimu vya Juu nchini ambapo Chuo Kikuu Mzumbe kwa mwaka huu 2019 kimeshiriki maonesho ya 43 ya Kimataifa Sabasaba, ambapo mbali na kutangaza programu zake imeshirikisha wanafunzi wabunifu ambao kupitia mafunzo ya Biashara wanayoyapata chuoni hapo wamekubuni biashara na kufungua makampuni mbalimbali wakitekelezs kauli mbiu ya mwaka huu ya " usindikaji wa mazao ya kilimo kwa maendeleo endelevu ya viwanda"
Mbali na bidhaa kupitia kitivo cha sayansi na teknolojia wanafunzi kwa kushirikiana na wakufunzi wao wamefanikiwa kubuni mfumo unaojulikana kama TraSMS-Cargo ambao utahusika kurahisisha uchukuzi wa mazao na bidhaa za kilimo kutoka kwa wakulima kwenda kwa walaji. TraSMS-Cargo ni mfumo wa kielektroniki unaowakutanisha wa wachukuzi na wasafirishaji kwa Lengo la kurahisha na kupunguza gharama za usafirishaji.
Morice Daudi Mhadhiri wa Kitivo cha Sayansi naTeknolojia chuo kikuu Mzumbe akionesha picha ya mchoro unaoonyesha mfumo wa TraSMS-Cargo uliobuniwa na wanafunzi na wakufunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe leo katika maonesho ya 43 ya Kimataifa Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wananchi akipata maelezo ya bidhaa kutoka kwa Jasinta Msamula mhadhiri wa Shule ya Biashara Chuo Kikuu Mzumbe leo katika maonesho ya 43 ya Kimataifa Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Bi. Fatna Mfalingundi Afisa Habari wa Chuo Kikuu Mzumbe akitoa maelezo kuhusu shughuli za Chuo Kikuu Mzumbe kwa mmoja wa wananchi aliyetembelea banda la hilo leo katika maonesho ya 43 ya Kimataifa Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Chuo kikuu Mzumbe wakiwa wamejipanga kwenye banda Lao tayari kuwahudumia wananchi wanaofika kupata huduma.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...