Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, amekutana na sekretarieti ya Yanga na kuzungumza masuala mbalimbali ya maendeleo ya klabu hiyo.

Kikao hicho kimefanyika leo Ikulu  ya Zanzibar na kuutaka uongozi kusimamia vyema rasilimali za Klabu na kudhibiti wadokozi wanaojinufaisha kwa maslahi yao. Balozi Idd ameweza kuupongeza uongozi wa Yanga kwa jitihada na mikakati ya kujikwamua kiuchumi ili kuepuka kuwa tegemezi kwa wafadhili. 

Amesema Yanga ni klabu kubwa lazima ionyeshe mfano kwa klabu zingine katika kila jambo na kwa upande atachangia Milioni 2 kwa ajili ya maendeleo ga klabu.Awali Mwenyekiti wa Yanga Dkt Mshindo Msolla alimueleza Balozi Idd juu ya miakati mbalimbali ya uongozi mpya wa Yanga katika kuijenga klabu iweze kujitegemea kiuchumi.

Pia, Dkt Msolla ameweka mkakati wa uongozi wao ni kuifanya Yanga kuwa timu yenye ushindani ndani na nje ya Tanzania. Yanga wamezindua wiki ya Mwananchi Visiwani Zanzibar hapo jana kwa kutembelea kaburi la muasisi wa Klabu hiyo na Rais wa Kwanza wa Zanzibar  Hayati Abeid Aman Karume pamoja na kucheza mechi ya kirafiki.

Matukio mengine ya wiki ya mwananchi yanaendelea kwenye maeneo tofauti tofauti, matawi na wanachama wa Yanga wakijitoa katika shughuli za Kijamii.Kileke cha siku ya mwananchi kinahitimishwa Agost 4 mwaka huu kwa Kikosi cha Yanga kutambulishwa rasmi kwa wachezaji wapya na kucheza mchezo wa Kirafiki na timu ya Kariobang Sharks ya nchini Kenya.
Makamu wa Pili za Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akimkabidhi Mwenyekiti wa Yanga Dkt Mshindo Msolla kiasi cha shilling Milion 2 kama mchango wake katika klabu hiyo baada ya kukutana nao na kufanya mazungumzo kwa manufaa ya Klabu ya Yanga.

 Mwenyekiti wa Yanga Dkt Mshindo Msolla akielezea jambo kwa Makamu wa Pili wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd wakati wa mazungumzo yao walipokutana leo Ikulu Zanzibar.

 Makamu wa Pili wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akizungumza na uongozi wa Yanga ukiongozwa na Mwenyekiti Dkt Mshindo Msolla baada ya kufanya nao mazungumzo ya kimaendeleo pamoja na kuwachangia shilling Milion 2
 Makamu wa Pili wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa Klabu ya Yanga ukiongozwa na Mwenyekiti Dkt Mshindo Msolla.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...