Afisa mkuu wa fedha benki ya NMB, Ruth Zaipuna (wa kwanza kushoto) akimkabidhi mfanyabiashara cheti kilichotolewa na benki hiyo kwa baadhi ya wafanyabiashara wa kupigiwa mfano. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya NMB, Donatus Richard akishuhudia. NMB imewakutanisha wafanyabiashara mbali mbali kwenye Kongamano la Klabu ya Biashara ya NMB mkoa wa Singida kutoa elimu ya biashara.
Afisa mkuu wa fedha benki ya NMB, Ruth Zaipuna (wa kwanza kushoto) akimkabidhi mfanyabiashara cheti kilichotolewa na benki hiyo kwa baadhi ya wafanyabiashara wa kupigiwa mfano. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya NMB, Donatus Richard akishuhudia. NMB imewakutanisha wafanyabiashara mbali mbali kwenye Kongamano la Klabu ya Biashara ya NMB mkoa wa Singida kutoa elimu ya biashara.


Benki ya NMB imejipanga kuhakikisha wafanyabiashara wa ngazi zote wanakuza mitaji yao, itakayowawezesha kuajiri Watanzania wengi na hivyo kupunguza makali ya uhaba wa ajira nchini.

Pia waajiriwa hao kupitia kodi watakazolipa, zitachangia kukuza uchumi wa Taifa .

Hayo yamesemwa juzi na Afisa mkuu wa fedha benki ya NMB, Ruth Zaipuna, wakati akizungumza kwenye kongamano iliyohudhuriwa na wanachama wa NMB Business Club mkoa wa Singida. Warsha hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Katala Beach Hotel mjini hapa.

Akifafanua, alisema NMB ina business Clubs 36 nchi nzima, na kila moja ina wanachama kati ya 150 na 300.

“Kundi hilo kubwa la wanachama limekuwa likifaindika na mafunzo mbalimbali tunayotoa. Mafunzo hayo yanajumuisha na bidhaa zinazotolewa kwao na Benki yetu,ikiwemo jinsi ya kutunza vitabu vya mahesabu. Vile vile elimu ya masoko na elimu ya mlipa kodi, ambayo tumekuwa tukifanya kwa kushirikiana na TRA”,amesema Ruth.

Akifafanua zaidi, afisa huyo amesema lengo ni kuhakikisha wafanyabiashara wote wanakuza mitaji yao.Aidha, amesema shughuli za wafanyabiashara wadogo na wa kati (MSMEs) ni muhimu mno kwa uchumi wa Taifa letu.

“Uchumi kwa ujumla wake, unategemea mafanikio ya hizi MSME. Nasi tunajivunia sana kuona kada hii ya biashara imeendelea kukua kadri siku zinavyokwenda. Hayo ni mafanikio makubwa sana, na ya kujivunia”,alisema.

Kwa mujibu wa Afisa Zaipuna, jumla ya wafanyabiashara 200,00 wadogo na wa kati (MSMEs) nchi nzima,mikopo yao inafikia thamani ya shilingi bilioni 600.

Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha biashara NMB,Donatus Richard,amesema lengo la kuwaunganisha au kuwakutanisha wafanyabiashara hao zaidi ya 200 kwenye warsha hiyo,ni wao kufahamaiana na kupeana uzoefu wa biashara za aina mbalimbali.

“Lengo mahususi kuwa na klabu hizi,ni kuendeleza mahusiano na wateja wetu.Mahusiano haya yamesaqidia mno benki kukua.NMB ikiendelea kukua,biashara nazo zinakua kwa kiwango kikubwa”,amesema Richard kwa kujiamini.

Wakati huo huo,mfanyabishara wa mabasi (Dubai express) Evans Makundi,ametumia fursa hiyo kuipongeza tawi la NMB mkoa wa Singida,kwa madai halina urasimu katika kupata mikopo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...