Pichani chini ni Matukio ya picha mbalimbali zilizopigwa katika Bandari ya Port Bell (Kampala) nchini Uganda,kwenye Hafla ya upokeaji wa Meli ya mizigo MV Umoja iliyobeba mabehewa ya treni kutoka Mwanza kuja Uganda ikiwa na mizigo ya World Food Programme. (WFP).
Katika Hafla hiyo Serikali ya Uganda iliwasilishwa na Waziri wa Nchi Uchukuzi General Katumba Wamala na kwa Upande wa Tanzania, Balozi wa Tanzania nchini Uganda alimwakilisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe.
Njia hii ya usafiri wa reli kutoka Dar Es Salaam hadi Port Bell (Kampala) Uganda, inapunguza gharama kwa asilimia zaidi ya 50 na pia inachukuwa siku 5 tu kwa mzigo kusafiri kutoka bandari ya Dar Es Salaam hadi Kampala.
Kwa mwaka jana WFP walisafirisha tani 40,000 na kwa kutumia njia hii wameokoa zaidi ya USD 2M.Ujumbe uluiosafiri na MV Umoja kuja na mabehewa yanye mizigo ya WFP walikuwepo
Mkurugenzi Mtendaji wa TRC Bwana Masanja Kadogosa, Eng Johnson Kisaka Mkurugenzi wa Uchukuzi kutoka katika Wizara na pia waliambatana na Bwana Michael Dunforf Mkurugenzi wa WFP nchini Tanzania.
Kwa upande wa Uganda timu ya WFP Uganda walikuwepo katika mapokezi ya meli na shehena ya mizigo wakiongozwa na Naibu Mkurugenzi Bi Julie Anne MacDonald.Hii ni njia nafuu na yenye tija katika kukuza biashara na matumizi ya bandari ya Dar Es Salaam na reli ya kati ambayo ni muhimu wafanyabiashara kati ya Tanzania na Uganda wanatakiwa kuichangamkia.
Dkt Aziz P. Mlima, Balozi wa Tanzania nchini Uganda akisoma Hotuba kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isack Aloyce Kamwelwe.
Kutoka Kushoto kwenda Kulia Bwana Michael Dunford ( WFP- Tanzania) Dr. Aziz P. Mlima ( Balozi wa Tanzania Uganda) na Bi Julie Anne MacDonald.
Mhandisi Johnson Kisaka akisalimiana na Gen Karumba Wamala.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...