MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imekusanya Sh. trilioni 15.9 kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ,kuanzia Julai Mosi mwaka 2018 hadi Juni 30,2019 kati ya lengo la Sh. trilioni 18.
Hayo yamesemwa leo Julai 31,2019 jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo wakati akitoa taarifa ya makusanyo ya kodi kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019.
Amesema katika robo ya nne ya mwaka huo wa fedha (Machi hadi Juni 2019), TRA ilikusanya Sh trilioni 1.1, Sh trilioni 1.2 na Sh trilioni 1.5 kwa mwezi Aprili, Mei na June.
Kayomb amesema katika mwaka huo wa fedha, Serikali ilianzisha mfumo wa stempu za Kodi za Kieletroniki (ETS) ambapo utekelezaji wake umefanyika kwa awamu mbili.
"Awamu ya kwanza, ilihusisha bidhaa za sigara, mvinyo, pombe kali, bia na Ain's zote za vileo, ambayo ilianza kutekelezwa Januari 15,2019 imeendelea vizuri na maandaalizi ya awamu ya pili ya utekelezaji wa ETS inayojumuisha bidhaa za vinywaji baridi, maji, juisi na bidhaa za filamu kama CD/DVDs," amesema Kayombo
Kayombo amesema mfumo huo wa ETS kwa awamu ya pili unatarajiwa kuanza kufanya kazi Agosti Mosi, 2019, kwa lengo la kukusanya kodi stahiki.
"Lengo Kuu la kubandika stempu hizi za kieletroniki ni kuongeza usimamizi na ufanisi wa ukusanyaji wa ushuru wa bidhaa ikiwa ni pamoja na kupata taarifa sahihi za uzalishaji viwandani ili kukusanya kodi stahiki,
" Ni matumaini ya TRA, wazalishaji, waingizaji, wasambazaji, wauzaji wote wa bidhaa zinazotozwa ushuru wa bidhaa pamoja na umma wataendela kutoa ushirikiano wa TRA ili kufanikisha utekelezaji wa mfumo huu kila mmoja kutimiza majibu wake kwa majibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizopo,"amesema
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...