Picha ya kwanza ni Diwani mpya Kassimu Gunda kata ya Likuyuseka wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma akiapa mbele ya Hakimu wa wilaya ya Namtumbo Gloria Lwomile.
picha ya pili ni Waheshimiwa madiwani wakiwa na diwani mpya wa kata ya Likuyuseka bwana Kassimu Gunda
NA YEREMIAS NGERANGERA …NAMTUMBO
Hakimu wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Gloria Lwomile amemwagiwa sifa kutoka kwa wananchi wilayani hapa pamoja na waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo kwa kutenda haki kizalendo katika kazi zake za kimahakama.
Wakiongeza mara baada ya kikao cha baraza la madiwani hivi karibuni katika ukumbi wa Hamashauri hiyo diwani wa kata ya Limamu Isdori Nyati na diwani wa kata ya Mgombasi Mrisho Mbawala walisema kuwa hakimu huyo ni msaada mkubwa kwa jamii hasa kwa kutoa miongozo ya kisheria kwa jamii hasa kwa kutumia muda wake mwingi katika kusaidia jamii .
Madiwani hao walisema wapo mahakimu wananchi wanawaogopa hata kwa kuongea nao na namna wanavyojiweka lakini hakimu huyo ni kimbilio la wananchi wilayani hapo hasa kwa kukubali kuongea na mwananchi wa kima cha chini mwenye tatizo na kumsaidia kisheria bila masharti yoyote walisema madiwani hao.
Madiwani walimwagia sifa hizo wakati hakimu huyo alipoombwa kumwapisha diwani mpya wa kata ya Likuyuseka bwana Kassimu Buruhani Gunda (CCM) aliyechaguliwa kuziba nafasi ya aliyekuwa diwani wa kata hiyo marehemu Ally Kombo.
Aidha Rashidi Kumbikila mwananchi wa mjini Namtumbo alidai kuwa hakimu huyo wa wilaya amekuwa kimbilio la wanyonge kwenda kupata ushauri wa kisheria hasa kwa kusaidia jamii ya watu maskini bure alisema mwananchi huyo.
Bwana kumbikila alidai amewaona mahakimu wengi katika wilaya ya Namtumbo lakini hakimu huyo hana makuu na hutoa ushauri kwa mtu yoyote anayehitaji msaada wa kisheria hasa kwa watu wengi maskini wasiona uwezo.
Mwandishi wa gazeti hili alimfuata hakimu huyo ili kuweza kuhojiana naye lakini alikataa kuongea chochote na badala yake aliingia kwenye gari na kurudi ofisini mara baada ya kumaliza kumwapisha diwani huyo mpya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...