Maonesho
hayo yameanza tarehe 28/06/2019 na yatamalizika tarehe 13/06/2019.
Wanachama wa mifuko yote miwili wanaalikwa kuja kupata huduma mbalimbali
katika banda namba 13.
NSSF
na PSSSF wanashiriki kwa pamoja katika maonesho hayo ili kuweza kutoa
huduma ya Hifadhi ya jamii ambapo NSSF inawahudumia wananchi kutoka
sekta binafsi na sekta isiyokuwa rasmi na kwa upande wa PSSSF
wanawahudumia wanawahudumia watumishi wa umma.
Wanachama pamoja na wadau wa Mifuko hiyo wanatakiwa kutumia fursa hiyo kutembelea banda katika viwanja vya sabasaba
Mabadiliko
ya mwaka 2018 katika sekta ya Hifadhi ya jamii yalifuta ushindani
katika sekta hiyo. Hivyo wananchi wanaandikishwa kwenye mifuko hiyo
kulingana na sekta waliopo.
Meneja
Kiongozi wa Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF Bi Lulu Mengele akitoa
elimu kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na NSSF katika banda la NSSF
na PSSSF katika maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika
viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa. 

Afisa
Uhusiano wa NSSF Bi Aisha Sango akitoa ufafanuzi kwa mgeni alietembelea
banda la NSSF na PSSSF katika maonesho yanayoendelea ya kimataifa ya
Sabasaba katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa. 

Meneja
Kiongozi wa Uhusiano na Elimu kwa Umma wa PSSSF Bi Eunice
Chiume akitoa elimu kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na PSSSF katika
banda la NSSF na PSSSF wakati wa maonesho yanayoendelea ya kimataifa
ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara
ya Kilwa. 

Afisa
matekelezo wa NSSF Ndugu Abdulaziz Abeid akitoa ufafanuzi kwa mgeni
alietembelea banda la NSSF na PSSSF katika maonesho yanayoendelea ya
kimataifa ya Sabasaba katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya
Kilwa.

Maafisa
Uhusiano wa NSSF (Aisha Sango, Kushoto na Amani Marcel, Katikati) na wa
PSSSF (Coleta Mnyamani) wakitoa elimu kwa wageni mbalimbali kuhusu
huduma mbalimbali zitolewazo na Mifuko hiyo katika maonesho ya kimataifa
ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara
ya Kilwa. 

Afisa
Uhusiano wa PSSSF ndugu Abdul Njaidi akitoa ufafanuzi kwa mgeni
alietembelea banda la NSSF na PSSSF katika maonesho yanayoendelea ya
kimataifa ya Sabasaba katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya
Kilwa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...