NA MWANDISHI WETU, MWANZA

MKUTANO wa 23 wa Taasisi zinazosimamia Mawasiliano kwa Nchi za Afrika Mashariki, (EACO) umeanza leo Julai 1, 2019 jijini Mwanza.

Sambamba na mkutamno huo pia wajumbe watashiriki Mkutano Mkuu wa 26 wa EACO ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Kuiweka Afrika Mashariki katika eneo la Uchumi wa Kidijitali".Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi, Atashasta Nditiye (Mb), ndiye aliyefungua mkutano huo utakaodumu hadi Julai 5, wenyeji ni Tanzania, pamoja na mataifa mengine ya EAC, ambayo ni Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudani Kusini. 
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (Mb), (wapili kushoto), akiongozana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasilkiano Tanzania (TCRA), Mhandisi James M. Kilaba (watatu kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya (TCRA), Dkt. Jones Killimbe (wanne kushoto) Afisa Mtendaji Mkuu wa EACO Dtk. Ally Yahya Simba (wakwanza kulia) na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Mawasiliano Bw.Mulembwa Munaku. (wakwanza kushoto), baada ya kufungua Mkutano wa 23 wa Taasisi zinazosimamia Mawasiliano Afrika Mashariki (EACO), utakaofuatiwa na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 26 wa EACO jijini Mwanza Julai 1, 2019
Muwakilishi wa Umoja wa Shirika la Posta Duniani (upu), Kusini mwa Afrika na Asia, Bi. Gladys Mutyavaviri ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu wa upu, akizungumza kwenye mkutano huo wakati wa ufunguzi.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James M. Kilaba, akizungumza na waandishi wa habari kufafanua baadhi ya mambo kuhusu mkutano huo.
Wajumbe kutoka Burundi, wakisikilzia hotuba ya Mhe. Naibu Waziri.
Wajumbe kutoka Kenya, wakisikilzia hotuba ya Mhe. Naibu Waziri.
Wajumbe kutoka Rwanda, wakisikilzia hotuba ya Mhe. Naibu Waziri.
Wajumbe wenyeji Tanzania, wakimsikiliza Mhe. Naibu Waziri Mhandisi Nditiye wakati akifungua mkutano huo.
Wajumbe kutoka Uganda, wakisikilzia hotuba ya Mhe. Naibu Waziri.
Mhe. Naibu Waziri Mhandisi Nditiye na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka mataifa wanachama wa EACO. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...