Marehemu Mpendwa Baba yetu, Joseph Mturi Mahemba 1949-2012)
Hatimaye siku, Miezi imepita hadi hii leo ambapo imetimia Miaka Saba (7) tangu ulipotutoka ghafla usiku ule wa siku ya jumatano ya tarehe moja ya Mwezi Agosti, 2012 na kutuachia huzuni kubwa.
Japokuwa haupo nasi hapa duniani lakini tupo nawe kiroho kwa kuendeleza mema yote uliyotufundisha na kutuasa.
Tunakukumbuka kwa Upole, Upendo, Busara na Ukarimu uliokuwa nao kwa familia na Marafiki. Mwongozo na matendo yako yataendelea kuwa dira kwetu
Daima unakumbukwa sana na Mkeo Rose Joseph, dada zako Theresia, Karaghita, Wankuru na Mnaga, wanao wapendwa Michael, Mkami, Niwa, Sagana, Mary, Geofrey, Nyakaho, Lecardia na Pricilla, wajukuu zako, pamoja na marafiki zako wote.
Ibada Maalum ya Maombi itafanyika tarehe 04/08/2019 Saa 3.00 asubuhi kwenye kanisa katoliki la Mt Maurus Kurasini, Dar es Salaam.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa jina lake libalikiwe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...