Mwalimu wa Kwaya ya watoto katika Shule ya Westminister Cathedral nchini Uingereza, Matthew Wright akikabidhi Optical Coherence Tomography (OCT) kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru katika shughuli fupi iliofanyika MNH leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa MNH, Dkt. Sufiani Baruani
Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Lawrence Museru akizungumza baada ya kukabidhiwa machine ya OCT na Mwalimu wa Kwaya ya watoto katika Shule ya Westminister Cathedral nchini Uingereza, Matthew Wright. Kulia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Macho, Dkt. Paul Nyaluke wa MNH. 
Pichani ni machine ya OCT inatumiwa na wataalam wa magonjwa ya macho kutambua magonjwa yaliopo katika pazia la macho (retina) ili kumsaidia daktari kuamua matibabu sahihi kwa mgonjwa.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Macho, Dkt. Paul Nyaluke akieleza jinsi machine ya OCT inavyotumika kutambua magonjwa yaliopo kwenye pazia la macho (retina) kwa mgonjwa mwenye matatizo ya macho.


Na John Stephen


Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepatiwa msaada wa machine ya kisasa ya Optical Coherence Tomography (OCT) ya kusaidia kupima magonjwa ya macho yenye zaidi ya thamani ya Shilingi milioni 100.

Msaada umetolewa na Shule ya Kwaya ya Westminister Cathedral ya nchini Uingereza kupitia Hospitali ya Mtakatifu Thomas iliyopo nchini humo kwa lengo la kusaidia wagonjwa wenye matatizo ya macho nchini. Mashine ya OCT inatumika kutambua magonjwa yaliopo katika pazia la macho (retina) kwa ajili ya kumsaidia daktari kuamua matibabu sahihi kwa mgonjwa wa macho.

Akizungumza katika shughuli fupi ya kukabidhi mashine ya OCT, mwalimu wa kwaya ya watoto katika Shule ya Kwaya ya Westminister Cathedral nchini Uingereza, Matthew Wright amesema watoto wa kwaya hiyo wenye umri kuanzia miaka minne hadi 13 wametoa msaada ili kusaidia wagonjwa wenye matatizo ya macho nchini.

“Mashine ya OCT itasaidia kutoa matibabu kwa maelfu ya wagonjwa wanaohitaji huduma, huu ni mchango wa watoto wa Shule Kwaya ya Westminister Cathedral ambao wamechanga fedha zao ili kutoa msaada huu,” amesema Mwalimu Wright.

Wright amesema mashine ya OCT pia itasaidia kutoa elimu kwa madaktari zaidi ya 20 wanaosoma jinsi ya kutoa matibabu kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa ya macho.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru baada ya kupokea msaada amemshukuru Mwalimu Wright pamoja na watoto waliochanga fedha ili kununua machine ya OCT.

Prof. Museru amesema mashine ya OCT itatoa mchango mkubwa kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na matatizo ya macho na ameahidi kwamba wataitunza ili iweze kufanya kazi kwa muda mrefu.

Pia, Prof. Museru amewataka wataalam kuhakikisha wanaitumia OCT kwa uangalifu wakati wa kuchukua vipimo kwa wagonjwa ili iweze kuwanufaisha watu wengi zaidi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...