Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imetupilia mbali mapingamizi ya Chadema na kupokea kielelezo cha Kamera ya kurekodi video na Tepu mbili kilichopingwa Mahakamani hapo na upande wa Utetezi katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa chama hicho akiwemo Mwenyekiti wao Freeman Mbowe.
Uamuzi huo umetolewa leo Julai 25, 2019 na Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba baada ya kupitia hoja za pande zote mbili.
Akitoa uamuzi huo, Hakimu Simba amesema, Kifungu cha 18 cha sheria ya ushahidi wa kieletroniki kimeweka vigezo vya upokeaji wa vielelezo vya eletroniki ambavyo shahidi namba sita Koplo Charles alikidhi vigezo hivyo na kuongeza kuwa, ushahidi wake umekidhi vigezo vyote vilivyohitajika kwenye kifungu hicho hivyo kwa muktadha huo mapingamizi yaliyowekwa na upande wa utetezi yanatupiliwa mbali.
"Mahakama imeyatupilia mbali mapingamizi ya upande wa utetezi, Kamera hiyo imepokelewa kama kielelezo namba nne na zile tape mbili kama kielelezo namba tano, " amesema Simba
Julai 11, mwaka huu Wakili Kibatala alipinga kupokelewa kwa vielelezo hivyo vilivyotolewa na shahidi wa sita wa upande wa mashtaka kwa kudai kuwa ushahidi wa kieletroniki hauwezi kupokelewa mahakamani mpaka kuwepo kwa kiapo mahususi juu ya utoaji wa vielelezo hivyo kwa mujibu wa sheria fungu la 18 na 19 ya ushahidi wa kieleketroniki.
Dk Zainab alijibu hoja hizo Julai 12, mwaka huu kwa kuieleza Mahakama kuwa aina ya utunzaji vielelezo vilivyowasilishwa na Shahidi wao ulikuwa mzuri kama yalivyo matakwa ya kisheria.
Katika kesi hiyo namba 112 ya mwaka 2018, Upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Wakili wa Serikali Mkuu Faraja Nchimbi, Wakili wa Serikali Mkuu Paul Kadushi, Wakili wa Serikali Mkuu , Dk. Zainab Mango na Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon.
Pia Upande wa utetezi uliwakilishwa na Wakili Profesa Abdallah Safari, Peter Kibatala, John Mallya na Hekima Mwasipu.
Mbali na Mbowe washtakiwa wengine ni Katibu Mkuu Chadema Dk.Vicent Mashinji, John Mnyika Naibu Katibu Mkuu (Chadema)-Bara na Salumu Mwalimu Naibu Katibu Mkuu Chadema Zanzibar.
Wengine ni Ester Matiko Mhadhini wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha)-Taifa pia Mbunge wa Tarime Mjini, Halima Mdee Mwenyekiti wa (Bawacha)-Taifa pia Mbunge wa Kawe, Ester Bulaya Mbunge wa Bunda Mjini, John Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini, na Peter Msigwa Mbunge wa Iringa Mjini.
Washitakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 13 likiwemo la kula njama na uchochezi
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imetupilia mbali mapingamizi ya Chadema na kupokea kielelezo cha Kamera ya kurekodi video na Tepu mbili kilichopingwa Mahakamani hapo na upande wa Utetezi katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa chama hicho akiwemo Mwenyekiti wao Freeman Mbowe.
Uamuzi huo umetolewa leo Julai 25, 2019 na Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba baada ya kupitia hoja za pande zote mbili.
Akitoa uamuzi huo, Hakimu Simba amesema, Kifungu cha 18 cha sheria ya ushahidi wa kieletroniki kimeweka vigezo vya upokeaji wa vielelezo vya eletroniki ambavyo shahidi namba sita Koplo Charles alikidhi vigezo hivyo na kuongeza kuwa, ushahidi wake umekidhi vigezo vyote vilivyohitajika kwenye kifungu hicho hivyo kwa muktadha huo mapingamizi yaliyowekwa na upande wa utetezi yanatupiliwa mbali.

Julai 11, mwaka huu Wakili Kibatala alipinga kupokelewa kwa vielelezo hivyo vilivyotolewa na shahidi wa sita wa upande wa mashtaka kwa kudai kuwa ushahidi wa kieletroniki hauwezi kupokelewa mahakamani mpaka kuwepo kwa kiapo mahususi juu ya utoaji wa vielelezo hivyo kwa mujibu wa sheria fungu la 18 na 19 ya ushahidi wa kieleketroniki.
Dk Zainab alijibu hoja hizo Julai 12, mwaka huu kwa kuieleza Mahakama kuwa aina ya utunzaji vielelezo vilivyowasilishwa na Shahidi wao ulikuwa mzuri kama yalivyo matakwa ya kisheria.

Pia Upande wa utetezi uliwakilishwa na Wakili Profesa Abdallah Safari, Peter Kibatala, John Mallya na Hekima Mwasipu.
Mbali na Mbowe washtakiwa wengine ni Katibu Mkuu Chadema Dk.Vicent Mashinji, John Mnyika Naibu Katibu Mkuu (Chadema)-Bara na Salumu Mwalimu Naibu Katibu Mkuu Chadema Zanzibar.
Wengine ni Ester Matiko Mhadhini wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha)-Taifa pia Mbunge wa Tarime Mjini, Halima Mdee Mwenyekiti wa (Bawacha)-Taifa pia Mbunge wa Kawe, Ester Bulaya Mbunge wa Bunda Mjini, John Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini, na Peter Msigwa Mbunge wa Iringa Mjini.
Washitakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 13 likiwemo la kula njama na uchochezi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...