Aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu(TFF), Jamal Malinzi,  Katibu wake  Selestine Mwesigwa na wenzao wawili wamekutwa na kesi ya kujibu katika mashitaka  20 kati ya 30 yaliyokuwa yakiwakabili ikiwemo ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji fedha.

Wengine waliokutwa na kesi ya kujibu ni  Mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga,  na Karani Flora Rauya huku Meneja wa TFF, Mariam Zayumba akiachiwa huru.

Uamuzi huo umetolewa leo Julai 23,2019 na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,Maira Kasonde kesi hiyo ilipofika kwa ajili ya uamuzi mdogo kuona kama washtakiwa wana kesi ya kujibu ama la.

Akisoma uamuzi huo, Hakimu Kasonde amesema, upande wa mashtaka ulileta mashahidi 15 na vielelezo tisa katika kuthibisha kesi hiyo.

Amesema katika mashtaka 30 waliyokuwa wakikabiliwa nayo, yapo pia mashtaka ya  matumizi mabaya ya madaraka dhidi ya Malinzi na Mwesigwa, shtaka la kula njama na kutoa nyaraka za uongo linalomkabili mshitakiwa Mwesigwa.

"Ni jukumu la mahakama kuangalia kama mshitakiwa ametajwa kwa namna yoyote katika mashitaka na ni upande wa mashitaka ambao wanatakiwa kuyathibitisha bila kuacha shaka yoyote mashtaka yote, katika ushahidi wote uliotolewa mahakamani dhidi ya shtala la kula njama, hakuna chembe ya ushahidi kwamba mshitakiwa Malinzi na Mwesigwa walikula njama kufanya makosa ya kughushi hivyo, ili kuthibitisha upande wa mashitaka ulitakiwa kuleta vielelezo vya kuonesha namna njama zilivyofanyika kwa.mantiki hiyo mahakama inawaona washtakiwa hawana kesi ya kujibu kwenye shtaka hilo."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...