Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
RAIS Dkt. John Joseph Magufuli  na Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar  Dkt. Ally Mohamed Shein wanategemewa kushiriki katika  wiki ya viwanda itakayofanyika nchini kuanzia Agosti 5 hadi 9 mwaka huu ikiwa ni katika kuelekea mkutano mkuu wa 39 wa SADC utakaofanyika nchini Agosti mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Waziri mwenye dhamana ya viwanda na biashara Innocent Bashungwa amesema kuwa mkutano huo ni fursa kubwa kwa watanzania wakiwa wanachama hasa katika kutumia fursa hiyo katika kutangaza huduma na bidhaa hasa za viwanda na utalii zinazopatika nchini kupitia mkutano huo.

Amesema kuwa Ufunguzi wa mkutano huo utafanyika Agosti 5 ambapo Rais Magufuli atakuwa mgeni rasmi na utafungwa Agosti 8 na Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ally Mohamed Shein na hiyo yote ni kutokana na uzito wa tukio hilo ambalo limebeba  faida kubwa kwa taifa na watanzania.

Bashungwa amesema kuwa "lazima tunufaike na mkutano huo tukiwa wanachama na ninawahimiza wenye viwanda wazidi kujitokeza kwa wingi zaidi, ninafurahi watanzania wanachangamkia fursa hii ambapo hadi sasa idadi ya washiriki waliojiandikisha wamefika 580 huku idadi ya watanzania ikiwa juu zaidi" ameeleza Bashungwa.

Aidha amesema kuwa wizara ya viwanda kwa kushirikiana na Wizara nyingine itaendelea kuhakikisha inawawezesha vijana ili kuweza kujenga uchumi wa viwanda unaowahusisha watu wa kada zote na kuahidi kusimamia vyema mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji.

Mkutano huo wa 39 wa jumuiya ya maendeleo wa nchi za kusini mwa Afrika unatarajiwa kufanyika Agosti 17 na 18 ambapo wakuu wa nchi 16 watakutana na Rais Magufuli ambaye ni Makamu mwenyekiti wa umoja huo atakuwa mwenyekiti kwa muhula mmoja kwa kupokea kijiti kutoka kwa Rais wa Namibia.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa akielezea faida za maonesho ya wiki ya viwanda kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) yatakayofanyika Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere kuanzia Julai 5 hadi 8, 2019 ikiwa ni sehemu ya matukio yatakaofanyika kuelekea mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa SADC.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa akisisitiza kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha ujenzi wa uchumi wa viwanda unaleta matokeo chanya hapa nchini na katika mataifa wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...